Genuine Nordic Vodka

Genuine Nordic Vodka

Wednesday, May 10, 2017

WHY,WHY,WHY DID THIS HAPPEN!!


Leo ntaongea na wazazi kwani hizi schoolsystem zetu na baadhi ya mentality and attitude ndio zinasababisha vitu kama hivi vitokee.
Not so long ago tulimjadili yule mtoto aliyechangiwa kupigwa na walimu na kila mtu aliguswa na kufoka but tuongee ukweli how man of you hampigi watoto?
How many men nchi hiyo hawapigi wanawake let alone wake zao ambao ni mama watoto za watoto wao?
Ukitaka kupoint na kukemea lazma tuanze na attitude zetu na malezi ambayo wengi wamepitia kuwa mtu kukufunza adabu ni lazma upigwe je hilo ni sahihi au?
Imefika mahala mtu unaacha mtoto wako shule kujua kwamba yuko safe,yuko kwenye mikono ya wakubwa but mnajua kweli mnawaachia Kina nani malaika wenu?
Ma school bus yanajazwa watoto kama mbuzi je kwani haya yameanza Leo?
Watu mnalipa maada makubwa so WHY not kukemea usalama wa watoto wenu.
Mara nyingi naona maschoolbus watoto hawajavalishwa a SEAT belt,SEAT belt saves lives ndiomaana ya kuwekwa kile kitu kwenye gari hilo nalo hamuelewi au?
Ma daladala yanaacha watoto sijawahi ona hata siku moja wakubwa mmeshuka kuwatetea watoto ndiokwanzaa mnaendelea na yenu.
School system mtoto anakaa mbagala anapelekwa kusoma kigamboni is that fair? Siku moja nawakuta watoto barabarani nawapakia nawauliza wananiambia dada sometimes yasipopita private cars tunakaa hadi usiku kusubiria usafiri na wewe mzazi uko nyumbani mpaka giza hivi kweli hiyo ni haki?
Huyu mwalimu kumuuwa Huyu mtoto si kitu kimeanza Leo kwani ilikuwa ndio adhabu yake yakuwapa watoto ni kuwafungia kabatini.,
A grown man has killed a child and all we can do nikuuliza why maana kakimbia na hatujui hata yukowapi na due to our system Huyu Huyu kiumbe anaweza baada ya mwaka akaibuka shule nyengine na kufundisha yet again, Sad!
Walimu wanapiga watoto,nishaona mwalimu akichukua pesa za mtoto akanunue soda na mengine mengitu aisee Amkeni wapendwa.
Kama mzazi wa mtoto Nyie ndio watetezi wao,Nyie ndio sauti zao NO matter what
Hiki kitendo ni cha kukemewa laasivyo mtazika wengi na hii ni moja tuloisikia what about waliofariki na hatujui malaika hawa jamen kisa mwalimu?..,
Acheni kuwapa Walimu so much power overwatoto wenu kwani wao Pia ni binadamu na AT Times wanafanya vitu ambavyo sio sahihi na kwenye hili mpaka kuuwa mtoto,Nimemaliza.com!

4 comments:

Anonymous said...

Nuru wakati nasoma saint kayumba long ago niliwahi kufungiwa stoo toka saa tatu asubuhi mpaka saa mbili usiku (bila kula)na mbaya zaidi mwalimu alinisahau kwamba amenifungia humo hivyo akaondoka akaja kukumbuka huo usiku. Natoka shuleni kufika nyumbani nakuta mama yangu kalia mpaka BP imepanda kalazwa hospitali, kaka zangu ndio wanahangaika kunitafuta. Na pia kumbuka nilienda mwenyewe nyumbani na sikupelekwa na mwalimu, baada ya mama kutoka hospitali alienda shuleni kutaka kujua kilichotokea waalimu na mwalimu mkuu wakamshambulia kwa maneno na kumwambia kuwa wazazi kama yeye ndio wanaharibu watoto na kumtaka mama anihamishe shuleni kwao. Nikahamishwa faster maana alisema mnaweza kuja niulia mtoto, sio wazazi wote wenye uwezo wa kusimama kwa watoto wao. Na uongozi wa shule na serikali za mitaa zinalea adhabu kama hizi ambazo hazina vichwa wala miguu na kuona watoto hawana haki mpaka tatizo litokee ndio wanajidai kupaza sauti. Sorry kwa gazeti ila imenikumbusha mbali sana. Winnie

Anonymous said...

Yaani nimeudhik mpaka nkasikia kutapika! Na huyu mwalimu awrkwe kwenye hiyo safe mbwaaa kabisa!

NURU THE LIGHT said...

Walimu kulindana ndio zao maana keshokutwa atafanya mwengine kwahiyo lazma wa back eachother hata kama wanajua kuwa wamekosea.,
Huoni issue hii alibaki mmoja tu na akaripoti atleast wakasave one life.
Bila hata pole gazeti lilikuwa zuri na by sharing umetufunza na mama yako alikupigania even though The system failed you n her

Wazazi mna power especially hizi shule mnalipa hela nyingi you have alot of power mkiwa kitu kimoja laasivyo mtazika wengi kwa vitu ambavyo mfumo unaweza kubadilishwa
This kitu haianzi shule but iko km ulivyosema within The system..
Am glad you are ok ila hawa walimu wengine wanatesa sana watoto wa Watu.
Thank you for sharing your story anonym 3.44

Cute Olive said...

Jamani roho imeniuma sana why lakini pamoja na adhabu lakini pia kuna ubinadamu kwamba kitu hiki ni sahihi kwa ninayemfanyia na anajua kabatika hakuna hewa kwanini tunaomba serikali ishukue hatua stahiki atafutwe popote aliko aisee.

Wazazi tunanafasi kubwa ya kuwalinda watoto wetu na majanga kama hayo maana bila mtoto shule haiwezi kuitwa shule so wazazi kwa umoja wetu tukemee mambo haya na katika vikao vya shule tusisitize usalama wa watoto haswa kwenye haya magari.