Genuine Nordic Vodka

Genuine Nordic Vodka

Tuesday, May 2, 2017

THEY DON!T WANT US TO BE GREAT POINT BLANK PERIOD!!!

 huyo kwenye simu tulikuwa nae kimwili tyuu..,


 A Lil Milkshake never hurt nobody.,.,

 Yummy

Wakipiga kelele ongeza spidi.
Wakipiga kelele ongeza juhudi.
Wakipiga kelele kaza mwendo.
Wakipiga kelele kataa uwoga na ongeza ushujaa.
Kelele zisiwe kisingizio wewe kutofanya.,
Kelele zisiwe sababu ya wewe kusema haiwezekani kwani mifano hai ipo na unaiona.
Kelele zisikufanye ukatike moyo bali zigeuze na kuziona kama uhamasishaji.
Kelele zipo kama ukumbusho kuwa unakaribia malengo yako kwani ulisikia wapi mvivu akipigiwa kelele?
Kujitambua si kitu huja tu bali ni safari na wengine bado hawajaanza hiyo safari so cha msingi ni kuelewa kuwa unachokiona wewe si kile anakiona mwenzako.
Wote mnaweza kusoma kitabu kimoja ila perception Zenu zikawa tofauti.
Kuna watu kazi yao ni kuamka na kutukana wengine kila kukicha lakin kwavile kwake yeye anajiona yuko sawa je wewe ni nani kumwambia hayuko njia sahihi?
As long as people watakuwa na jukwaa kwa kutukana au wakifanya mabaya juu ya watu basi kamwe hawawezi jiona kuwa wanakosea na Sometimes wallopo jukwaani na kutizama na kushangilia hao ndio wabaya zaidi.
Kuna wasiofaham na kujua uchungu wa mwenzao mpaka yawakute.,
Kuna wanaojua uchungu na maumivu ya wenzao na bado wanafurahia kwani hiyo ndio faraja yao.
Katika maisha muogope sana mtu ambae ameshagive up na maisha yake kwani hana lolote la kuhofu tena au kuogopa tena meaning anaweza kufanya chochote kwa yoyote mda wowote.
Jaribu kuona maisha yako mbali na sio ya leo tuu basi utakuwa motivated sana trust me on this.
Katika maisha Jua kwamba Wewe ndio Mchoraji wa ramani na safari ya Maisha Yako so Chora ramani ambayo itakutangaza wewe Vyema si kwako tu bali hata kwa wale waliokuzunguka,Nimemaliza.com!!!


3 comments:

Cute Olive said...

Kabisa Nuru umeongea yote ukisikiliza ya watu wanacomment nini juu ya maisha yako kweli utapotea wakipiga kelele zao ni kusonga mbele kwa mbele wakija kushangaa umewaacha njia panda!

NURU THE LIGHT said...

HASWAAAA.,,

Anonymous said...

Sumu sio kwa ujumbe huo maisha yanaendelea. Usinichoshe