Genuine Nordic Vodka

Genuine Nordic Vodka

Monday, July 3, 2017

A GIVEAWAY!!!Hiki kiatu ni size 4 na ni kipya kabisa...
Mimi hakinitoshi niliorder online sasa kinakaa tu why..
Kipo kwa anayekitaka,drop a comment on why kije kwako,Legooooo!!

29 comments:

Anonymous said...

Hi Nuru,I am one of your oldest readers/followers for more than 8years,there's no day I don't log into your blog and even a day like today I do so for more twice/thrice a day.I enjoy your blog simply because we share a lot in common; from Fashion,Lifestyle, By always Creating a platform for new talents esp. those that are rarely noticed, a few interesting gossip news to keep us up-to-date, last but not least I admire how loving and passionate you are towards your family members including us your readers if I may categories us that way I guess LOL. I think I well deserve the shoe for being a LOYAL reader for all those years just to compassate my internet bundles and time (Just Kidding) Not to mention I'm a size four,so kindly consider me and if am correct am the first to comment so why not..... P.K

Anonymous said...

oh PK you deserve it, my vote goes to you, your views on this blogs are like mine...(secret followers/admirers of the blog we share something in common.....SJL

comfort said...

Asante Nuru me ukiniambia size 4 hata sielewi mwenzio.

Irene said...

kwakweli hiki Nuru kinipite mana unaweza nivunja na pili nakupenda sana ila namiguu ya kiume so wacha wenye small size wapate

NURU THE LIGHT said...

Size 4 ni 37 Comfort...
So far PK uko nr 1 na ikifika monday by jioni nitatoa nani ni.mshindi so legooo.
And ya PK thank you for being a loyal reader and all of those who have been with me from the start...Nawapenda

NURU THE LIGHT said...

Irene na nyie nitawafikiria mgao mwengine ntatoa vya chini...

comfort said...

Nilivyo nalimguu likubwa sasa mmmmh hatahakinitoshi mwee napishana nazawadi hivihivi jmn

Anonymous said...

NURU, kwanza nilianza kupenda mziki wako from walimwengu to msela baada ya kukufuatilia i came to learn kuwa una blog since then i have never missed a day bila kupita humu (na siku hizi bundle ni majanga ila navizia hata ofisini). sijawahi kukutana na ww ila picha zinaonyesha unapenda kucheka and to have a lot of fun something which i love too. i love how you guys dance na kina MIKEY MIKEY so freely like its nobodies business, i love your sense of style especially your shoe game(winkwink).
kuna kipindi ulipumzika blogging ulinipa shida sana sasa nikawa najiuliza whats wrong with her, nilipata tabu na sikuwa na namna ya kukuuliza manake hata facebook nlikua sikuoni. if at anytime umewahi kuwaza kuacha blogging please dont, you inspire soo many of us and teach us the importance of living life and enjoying it to the fullest. by the way huwa naenda sana changani beach kigamboni huwa nasema siku nikukutana na wewe utajutraaaa if i dont deserve this pair of shoe please promise to bear with me nikikuona mtaani. lol

Anonymous said...

nimefunguka hadi i forgot to write my initials haha, its H.S.

Bintinyota said...

hehehehe napenda hills kufaaaa
lakini wacha tu mdau wa kwanza achukue japokuwa hizo rangi ni maradhi yangu.

na humu wengine siye wakongweeee kama wewe PK. lakini you deserve it.

ester lewis said...

Kiatu ni kizuri sana nuru, pia ntafurahi kama kikija kwangu cz nina harusi ya dada yangu next weak hope ntapendeza

Cute Olive said...

Kiatu kizuri mmnooooo Nuru Mungu aendelee kukubariki maana kutoa ni moyo sio wote wana roho hiyo.

Anonymous said...

mimi licha ya kuwa msomaji wako wa muda mrefu ila pia ni wifi kivuli wako kwa kaka ako Dreidel manywele.

Anonymous said...

Thanks Nuru,Much Much appreciate.. Am crossing my fingers till Monday,God Bless. P.K

Anonymous said...

Thank You SJL. I much appreciate the love and the vote,God Bless.

anonymus said...

Hi nuru size yangu hiyo..sababu tosha..kuhusu kuanguka nitakamatia miti na ukuta nikitoka kwenye gari!mwamini

NURU THE LIGHT said...Mwamini hahahahahah i can't with you,,,

H.S muwe mnaongea maana kuna wakati i think of stopping but thank you cause you remind me of why i am doing it...,

Ester jumatatu jioni natoa jibu..,

Wifi kivuli umetishajeeeee hahahah

Comfort usijali migao mpaka mwaka uishe ucjali love..
Bintinyota ytko special inakuja sala usihofu..

Anonymous said...

Hahahahahahaaa nimecheka kwa sauti na nimepata raha pia. Kwa mtazamo wangu nadhani mdau wa kwanza kinamstahili jamani ni kura yangu tu wapendwa, anaitwa P.K wengine sisi na uzito huu wa gunia la vitunguu unaeza vunjika kiuno halafu ukashindwa kutekeleza majukumu ya usiku (joke). Ila kizuuuriii hichooo. Wifi kivuli you made my day. Winnie

Bintinyota said...

hahahahaha miye walaaaa sina hofu!!
najua wakubwa huachia wadogo kwanza, hahahahahah

honestly kwa maelezo ya wadau wawili humu ndani they deserve it.

Allah Barik

sosoano said...

hahahah!!!!!!!! da nuuu we balaaa
nimependa watu wamejua kujielezea kwelikweli
mie niko na kimguuu mana navaliana hata na mtt wa darasa la sita jmn,

Anonymous said...

Mie kwanza ni mamdogo. pili nina mguu mkubwa but tatu and the most of them all, ni kukushukuru kwa kuwakilisha duniani the DNA of giving that our kaukoo is blessed with.

Keep that mwenge wa utoaji shining bimdogo and you will continue seeing them blessings overflowing kama hivyo ulivyo na zaidipo.

God bless you na siku nyingine kwenye mgao wa flatties na number kubwa nitajifaragua. maana umri nao umetutupa mkono mambo ya kunin'giniza vigimbi hewani tumesha bow out.
Mgee tu P.K

Pwenty of love,
Mamdogo wa Boston

conn4heaven said...

Mi nampenda Nuru bure hata kama sijapata kiatu

Christine Mhanusi said...

Nuru the nimekuwa nikikufalitia sana, the first time nilikuona ulikuwa unafanyiwa interview enzi hizo siku nyingi kama sikosei ni ITV ama EAT ukiongelea maisha yako na familia yako pia ukaelezea umri wako naukumbuka kabisa mpaka mwaka uliozaliwa nilianza kukupenda na kukufatilia sana kwasababu unajua ku keep na kumaintain mwili wako, pia nilikupenda sababu ulikuwa unaongea kiswahili kilichonyooka sana sio cha maringo kwa sababu umekaa sana nje ya nchi. Huwa sio mtu wa ku comment sana kweny blog yako ila leo nimeona niseme tu mimi ni shabiki wako namba moja toka hizo enzi, navaa namba 37 but hata nisipopata bahati ya kupata nitafurahi kwa wengine.

NURU THE LIGHT said...


Thank you Christine for your kind words...Maneno mazuri na yamenifariji..
Ahsanteni woteeee mlochangia..mmetisha sana
kwavile wengi wamempigia kura P.K the shoes will go to her..
P.K viatu ni vyako sasa sijui uko wapi...
kama upo tz itabidi ustahamili maana sivitumii mpaka nimpe mtu siamini kabisa hata DHL nilituma vilifika nusu so utanisamehe mpaka nimkabidhi mtu kama nilivyofanya kwa Cute Olive na Suzana na wakavipata..
hongera P.K na nijulishe uko wapi na nawasiliana vipa na wewe sitopost hiyo comment,,shukran kwa wote!!!

anonymus said...

Hongera sana P.K....na Nuru uzidi kubarikiwa.!

sosoano said...

hongera sana P.K
and again da nuu Ubarikiwe kwa moyo wako
ila sasa kwa hili ndio nimeona na hata wasioonekanaga

mischa said...

Hongera PK.

Mm hata mchuchumio sivai,next giveaway ntashindania lazima.

Irene said...

mh hii post kiboko imefikisha comments 27 majanga

Anonymous said...

Asanteni sana kwa wale wote walionipigia kura kwa namna moja au nyingine. Kwa kweli nimependa sana ukarimu wenu wa dhati. Hii ni kiashirio tosha sisi sote ni LA FAMILIA kwenye hii blog. Mungu awabariki na nina imani kuwa kuna kila zawadi kwa kila mdau. Mwenyezi Mungu azidi kubariki kazi ya Nuru the Light na zaidi kumuongezea pale alipopungukiwa. Asante sana Nuru na wadau wote kwa ujumla. Hii post imevunja rekodi ya comments nyingi kwenye blog na sifa na utukufu ni kwa Mungu pekee aliye juu kwa kuniwezesha ushindi huu. Nawapenda wote kwa personalities zenu zinazo reveal through comments zenu. Huwa nacheka sana ninapo soma comment tofauti esp. nyingi zikiwa zakutia moyo na sio matusi na mashutumu kama blog zingine. Mungu azidi kuwabariki kwa kila itwapo leo. Mad Love-P.K