Genuine Nordic Vodka
Saturday, December 17, 2016
A FOOD FOR THOUGHT!!!
Ama kweli Duniani kuna watu na Viatu.
Ama kweli Duniani kuna Ndugu Na Ndugu jina tu.
Hivi kabisa umkute ndugu yako amekaa na mtu baki na kukuongelea uwongo au kitu cha kiuhater huyo ni ndugu au nuksi tu?
Hivi ndugu ambae ananyima ndugu wenzake na kuwawezesha huyo ni ndugu kweli?
Kuna ndugu wanaotaka kila kukicha wao ndio wawe juu tu na kuombwa na waliozungukwa instead ya kuwawezesha.
Leo ntamuongelea ndugu ambae sio wa damu bali ni mtoto aliyelelewa nyumbani na kiukweli mimi siwezi kuchukua sifa nisizostahili kwani sikumlea mimi.
Point is huyu kiumbe wiki hii nzima kanifanyia wema ambao sijui niuongelee vipi.
Kanionyesha utu ambao hauuzwi tena dukani bali hushushwa na malaika.
Ningependa kutoa shukrani zangu kwako kwani wako walio na zaidi yako bali hawakunifungulia mlango na kunikaribisha ndani,Thank you M!!!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
3 comments:
Undugu ni kufaana na si kufanana.
Mama yangu alikua anatuambia tukiwa wadogo Bado,KUA uyaone😶😶!!! Yote maisha,tushukuru Mungu kwa yote
Nuru Leo umenigusa!!!
Asante sana
Post a Comment