Genuine Nordic Vodka
Thursday, September 15, 2016
IT STARTS WITH A DREAM AND THEN A SIMPLE ACTION THAT LATER TURNS INTO A REALITY,TBT OF MY JOURNEY WITH THE KA-PLACE YOU BETTA RESPECT MY HUSTLE!!!
Leo naongelea kuhusu Kuwa na Nia na Njia bali unakuwa na Uwoga,,
Nimegundua watu wengi sana wana uwoga wakuinvest au kuanzisha biashara,,
Kiukweli sio kila mtu anaweza kuwa mjasiriamali na ndiomaana kuna watu watakuwa waajiriwa na hakuna ubaya wowote kuwa muajiriwa as long as uko happy,,
Kuna raha yake pia kuwa muajiriwa maana the only thing utakuwa na wasiwasi nao ni kufanya kile ulichoajiriwa meaning kazi yako na mengine yote kumuachia bosi wako,,
Kuwa boss haina raha tuu bali kuna responsibility that comes with it na sio kila mtu anaweza,,
Nikirudi kwenye SWALA la Uwoga kuna watu wanatamani lakini hawathubutu,,
kuna wenye uwezo na elimu ila ni wavivu na hawataki majukumu,,
kuna wenye means lakini uwoga umewatala au hawana support kutoka kwa mume,familia au jamii maana kuna sehemu msidhani kuwa mjasiriamali ni kitu positive maana kuna watu bado wanataka mwanamke awe tegemezi na sio wakujitegemea so humpa vikwazo ili asijiendeleze,,
Na pia kuna wanawake wenye Waume Zao wanaotaka wajishughulishe ila wamepata wanawake wasiotaka hilo,,
Kuwa muoga its natural ila jaribu kutoupa uwoga nafasi ya kutawala ili iwe kikwazo wewe kuthubutu
Na hii mentality ya mtu lazima uwe tajiri kuanzisha kitu itoweni kabisa akilini mwenu,,
Matajiri wengi someni historia zao walianza na kitu kidogo na kuja kuwa na Empire baadae,,
Jaribu kuwa na watu ambae mnashare ndoto zinazolingana maana A looser hawezi kutaka wewe ufanikiwe kama yeye alifeli,,
Wako watakaokuja na kutaka kukuonyesha njia sahihi na wako pia watakaotaka kukukata moyo,,
Wapo watakao kuunga mkono ukianza biashara yako na wako ambao watakukimbia,,
Utapata marafiki wapya wenye nyuso za wateja wako na hata kuwa na familia ambayo hukutarajia,,
Utapitia mengi ila kumbuka kuwa na subra,kuwa jasiri,kuwa mvumilivu na mkarimu na chochote kuliko vyote kutobagua MTEJA kwani MTEJA NI MFALME,Nimemaliza.com!!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
2 comments:
Hongera mwaya kwa uthubutu.changamoto kubwa inayotukabili wafanyakazi tunaofanya ujasiriamali ni kukosa wasimamizi wazuri na hata wafanyakazi wanaojielewa mfano watu wakuuza maduka na kusimamia mifugo.mwamini
Ni kweli kupata wafanyakazi bora pia ni mtihani hata mimi nimepitia si kitu rahisi kabisa,,Ahsante
Post a Comment