Genuine Nordic Vodka
Wednesday, February 3, 2016
MAULID NAKUGAWAAAAAAAA!!!
DADA ZANGU HUU NI MWAKA WA MABADILIKO
Umempata bwana
Umempenda kweli
Umemlalamikia kwanini hakupeleki kwa wazazi
Bwana akakupeleka kwa wazazi wake kukutambulisha
Siku ya kwanza umeshinda unachat..
Siku ya pili umeshinda unachat...wanak
utazama tu,
Siku ya tatu ukaambiwa sasa zamu yako kupika,vya huku unaweka huku..vya hapa unaweka pale..
Yani hujui kupika kabisa...sufuria unashika utadhani umeshika powerbank, unapika na lipstick,umevaa saa, umevaa ma culture msosi wa kula wakwe zako huwezi kupika..umevaa "MINISKIRT" hata wafanyakazi wa fastjet umewapiku
Ukiambiwa kuwa hufai kuolewa unavuta mdomo kama umenyimwa ubuyu...
Unaanza sema wakwe hawakupendi ...unalalamika weeeee
Unashindwa kuelewa kuwa wewe ndo tatizo..
Usitake kuolewa ukadhani mumeo atakuwa anakula chips na wewe utakuwa unakula Pizza kila siku.
Tambua hata kuchemsha chai basi ,jamani au unadhani Google wataleta APP ambayo unaweka USB kwenye simu unaielekezea kwenye sahani inaproduce msosi?
Tumia akili ndoa ujipange...
Usidhani ndoa ni kama kupiga picha huku umejibinua binua makalio...
Ni mtazamo tu, Take it O Leave it
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment