Genuine Nordic Vodka

Genuine Nordic Vodka

Friday, August 7, 2015

ONTO OTHER NEWS!!!


Baadhi wasanii na wadau wa tasnia ya burudani Bongo, walikuwa na hafla ya kumuaga na kumshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya M Kikwete, iliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jana.
Wasanii hao walimshukuru na kumpongeza JK, kwa kile walichokiita kutatua matatizo yanayoikumba tasnia ya burudani kwa kiasi kikubwa.
‘Well’ sasa leo kumeibuka sintofahamu, kutoka kwa wasanii wawili wakongwe wa ‘game’ ya Bongo Flava rapper Soggy Doggy ‘Hunter’ na RNB star Rama Dee, wakidai hafla hiyo haikuandaliwa na wasanii bali imeandaliwa na mtu ambaye sikuzote wanamtuhumu kuwa ndio anayehusika kuwagawa wasanii katika matabaka.
Kupitia kupitia ukurasa wake wa Instagram, Rama dee amebainisha hayo huku akisisitiza kuendelea kupigania haki yake kama msanii.Aliyewaweka wasanii pamoja jana ndie mwenye kuvuruga umoja wa wasanii siku zote, yupo nyuma ya wasanii” ameandika Rama Dee.
Nae rapper Soggy Doggy, amefunguka kuwa haimuingii akilini wasanii kugharamia shughuli ya jana Mliman City, wakati wengi wao wakiumwa hushindwa kufikisha hata milioni 2 ya mchango kwa ajili ya matibabu.
“Maswali ya kujiuliza kuhusu dinner iliyoandaliwa na umoja wa wasanii ambao haujawahi kuwepo
1.umoja huo umeanzishwa lini na viongozi wao wakina nani?
2. Wasanii wanatambua kuwa kuna umoja wa wasanii tena usiokuwa na jina?
3. Kama wasanii waliandaa kumuaga rais kwanini kulikuwa na rundo la viongozi wa chama tena wa chama kimoja cha siasa?
4.magufuli kapewa nafasi ya kipekee kaenda kama mgombea au waziri?
5. Nani aligharamia gharama za sherehe?
6. Wasanii wamepata wapi hizi pesa wakati wenzao wakiumwa wanaandaa matamasha na kuweka viingilio kuchangia na hawapati zaidi ya million 2?
7. Kwanini wasanii ambao ndio wanadai kumualika muheshimiwa rais waliandaliwa kadi ya mualiko badala ya wao kumuandalia muheshimiwa rais kadi ya mualiko?. Tafakari chukua hatua.” Ameandika Soggy.
Katika ‘line’ nyingine, wakongwe hawa wameshindwa kumuweka bayana Yule wanayemuita muandaaji wa hafla nzima ya jana.
Rama-3

No comments: