Katika kile kinachoonekana ni kuishiwa sera na kutumia ubabe na ukorofi ili kutetea nafasi yake ya kugombea ubunge wa Jimbo la Kongwa, Mheshimiwa Naibu Spika wa Bunge La Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Jimbo la Kongwa alipiga kwa gongo ambalo amekuwa akitembea nalo huku wasimamizi wa uchaguzi wakifumbua macho kitendo cha mgombea kutembea na silaha hiyo kwenye kampeni.
Inadaiwa na mtu aliyefuatilia kwa karibu tukio hilo mkutanoni kuwa Kuna mgombea mmojawapo (mkazi wa Kongwa aitwaye ngatunga) Alisimama kuuza sera zake na kudai kuwa Kongwa kuna madini jimbo halijafaidika na chochote kutoka kwa wachimbaji wa madini... Mara moja Ndugai alimtishia kuwa anyamaze la sivyo angemuonesha kazi kwa kile anachodai kuwa ni kuongea upuuzi..
Wakati wagombea hao wakiendelea kujibizana suala hilo ndipo ghafla mheshimiwa alipomuona Mmojawapo wa wagombea aitwaye Dr Joseph Chilongani ameshika simu na kutahamaki kuwa alikuwa akimrekodi kwa kuvunja taratibu.
Ndipo Job Ndugai alipoamka na kumwambia "Tena wewe nilikuwa nakutafuta siku nyingi sana, unanirekodi na makamera yako na leo utanitambua mimi ni nani."
Mara Ndugai akakusanya nguvu na kumpiga Dr Chilongani kwa fimbo hiyo. aidha hata baada ya kuanguka chini Ndugai alimfuata na kumrukia kumkanyaga tumboni akiwa na hasira na nia ovu ya kutaka kumdhuru zaidi..
Baadae wananchi walipata hasira na kutaka kumshughukilia kwa kichapo Mbunge huyo na ndipo alipopanda haraka gari lake haraka na kukimbi Eneo la Tukio..Inasadikiwa yule mgombea mwingine alijaribu kumnyanyua Dr. Pale chini, jambo ambalo baadhi ya wananchi walilichukulia ni kama kutaka kumdhuru zaidi hivyo walianza kumpa kichapo huyo mgombea mwengine kiasi hadi watu wengine walipoamulia..
1 comment:
This man is so emtional. Hata anapoongoza mijadala migumu ya bunge anatumia jazba muda mwingi badala ya busara tofauti ya Anna Makinda ambaye naye aliuwa na jazba lakini akakutana na machizi wa Chadema wakamweka sawa akawa anatumia busara na wakati mwingine kuwapotezea li maisha yaende maana aliona kazi itamuwia ngumu. Ila huju jamaa anajiona kama ndiye Rais maana mpk unawapiga wagombea wenzako mpk kuzirai kweli ni kichaa au uchu wa madaraka. Na nyie wananchi sasa ndiyo pumba zipi na mchele upi. lol
Post a Comment