Genuine Nordic Vodka

Genuine Nordic Vodka

Wednesday, July 29, 2015

UCHAGUZI 2015!!!


4 comments:

Anonymous said...

Makubwa haya ya Siasa jamani Mwenyezi mungu tunusuru Nchi yetu iendelee kuwa na Amani na tusipate viongozi mafisadi tena.

Anonymous said...

Huyu Mzee Lowassa jamani ni muongo hatari, kwanini anashindwa kusema ukweli kuwa deal la Richmond lilikuwa na la Msabaha (ambaye alikuwa waziri wa nishati wakati ule) pamoja na shemejie Mohamed Salehe? Kwanini anashindwa kuwaambia wananchi ukweli na kuomba msamaha kuwa Msabaha alimpotosha mpaka akafanya kinyume na maazimio ya baraza la mawaziri ambaye yeye ndie alikuwa kiongozi?

Mwakyembe alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati hakuwa Waziri lakini alikuwa mfuatiliaji mzuri sana wa issue za wizara hiyo.

Richmond ilikuwepo na ilikuwa ikisuasua na kuloby kupata kazi wizarani wakati hata mtaji walikuwa hawana, na walikuwa wakitaka kujenga bomba la mafuta kutoka Dar mpaka Mwanza (sijui kwa pesa ipi lol).

Yeye akiwa Waziri Mkuu alikuwa kiongozi wa Baraza la Mawaziri na kwenye kikao chao iliamualiwa kwamba Tanesco waende wakaongee na Globeleq (Kampuni ya wa UK iliyo na hisa Songas) kuhusu kukubaliana kupunguza tarrif na kufikia maelewano kwa sababu mradi huo ulikuwa ni wa muda mfupi na wa Ermegency. Tanesco na Globeleq walikuwa wako kwenye mazungumzo siku nyingi na hiyo process ilipofikia ilikuwa ni kupata baraza za baraza la mawaziri ili kuepusha nchi kuingia gizani kwa kukosa umeme.

Msabaha kama waziri wa Nishati alipewa kazi ya kufuatilia kuhakikisha kuwa Tanesco wanafanya kikao na Globeleq na kufikia muafaka wa kushusha tarrif. Lakini badala yake akawalazimisha Tanesco wafanye kazi na Richmond (sitaenda in detail hapa) Na alipata suport kubwa kutoka kwa Waziri Mkuu ambaye alishindwa kumwambia Msabaha afuate maagizo ya kikao cha baraza la mawaziri.

Matokeo yake jamaa akawa yeye sasa ndio anafuata ushauri na maelekezo ya Msabaha. Hata walipofika Wazungu wa Globeleq kutoka Marekani wakaenda ofisini kwa Msabaha badala ya yeye kuongea nao akawafukuza na walipotoka hapo ili waende kuongea na Waziri Mkuu, Msabaha akapiga siku kwake na kumwambia kuwa mie nimeshawafukuza huku kwangu wanakuja kwako, na kweli walipokwenda ofisini kwake na yeye akawafukuza. Na hapo ndipo Richmond ilipopata nguvu na baraka za Msabaha na yeye Waziri Mkuu.

Sijui kwanini watu ni wepesi sana wa kusahau au wanafikiri kuwa hakuna Mungu na ni rahisi kuficha ukweli. Haya lets say yeye hakuwa na chochote kwenye deal la Richmond kilichomfanya amsikilize Msabaha na akatae kuongea na Viongozi wa Globeleq ni kitu gani? Haya Msabaha alimislead kwanini hakuirudisha hiyo issue kwenye baraza la mawaziri na kuwaambia kuwa nimewafukuza Globeleq kwa sababu 1, 2, 3, na kuwaliza kama ni sawa wao kuendelea na Richmond.

Itaendelea comment inayofuata

Anonymous said...

Inaendelea kutoka comment ya juu

Mwisho kabisa wasimsingizie Rais Kikwete uongo wowote, baada ya hii issue kuanza kuandikwa magazetini Rais Kikwete alitamka kwenye kikao chake na Wahariri wakati akiongea na wananchi katika ratiba yake ya mwisho wa mwezi kuwa ataenda kukagua hiyo mitambo ya Richmond kama tayari wamekwishaanza ujenzi. Msabaha hakujua kama Rais Kikwete ataenda kweli akafikiri labda ni porojo tu za kuwaondosha njiani wahariri. Baada ya kikao kile siku 2 baadae Mheshimiwa Rais Kikwete akafanya ziara ya ghafla kwenda kukagua hiyo Richmond. Wakati huo hiyo Richmond ilikuwa haijafanya chochote hata nyasi tu kwenye eneo walilokuwa wamepewa na Tanesco zilikuwa hazijalimwa. Taarifa ya Rais kwenda kutembelea eneo la mradi lilifikishwa wizarani very late ikabidi watu wapelekwe site wakafyeke majani na kusafisha eneo usiku na kesho yake Mheshimiwa Rais alipokwenda site, aliagiza kuwa Richmond wasilipwe senti 5 mpaka kazi yao ionekane. Dili lilikuwa kuwa Richmond walipwe pesa na serikali kisha pesa hiyo ndio itumike kufanya kazi ya ujenzi na kununua mitambo wakati Globeleq walikuwa na uwezo wa kufanya hiyo kazi kwa capital yao ila kwa kuwa hiyo nayo ilikuwa ni kampuni iliyokuwa inamilikiwa na serikali ya nchi moja ya wazungu hakukuwa na uwezekano wa kupata mgao ndio maana ikakatwa.


Anyway Richmond ilikuwa ni emergency project tena ya muda mfupi lakini imeacha makovu makubwa kwa Watanzania. Watu wamuogope Mungu kwa kusema vitu wasivyovijua wala kuviona, na inawezekana Mheshimiwa kweli kumbu kumbu inapotea anaweza kukana hadharani kuwa hakumfukuza MD wa Globeleq aliyesafiiri kutoka US kwenda kuonana nae ofisini kwake kwa kufuata maagizo ya baraza la mawaziri kupitia Tanesco ya kurenegotiate tarrif. Ila ukweli siku zote una njia yake ya kutoka iko siku utatoka tu na watu wote watajua ni nini kilichokuwa kinaendelea.

Anonymous said...

So far Lowassa alikuwa nje ya serikali kwa miaka nane na hiyo miaka nane usanii na madudu yaliyofanyika serikalini ni unspeakable. That led me to believe Kuna mtu muhimu ambaye Alitakiwa awajibike na Lowassa lakini bado yupo kwenye nafasi yake. Lowassa kama mtendaji hawezi kukwepa lawama lakini bosi wake should also carry most of the blame. Huo ndio tunaita accountability.