Genuine Nordic Vodka

Genuine Nordic Vodka

Wednesday, July 8, 2015

ONE OF THE MOST DISSAPOINTING STATEMENTS I HAVE COME ACROSS BY TUNDU LISSU!!!


ASEMAVYO MH.TUNDU LISSU.
...Wajameni kila mmoja na heshima inayomstahili. Jana usiku niliahidi kutoa maelezo na msimamo wangu juu ya suala la kiinua mgongo cha wabunge tunachosikia tutalipwa mara baada ya kumaliza Bunge wiki ijayo. Nasema 'tunachosikia tutalipwa' kwa sababu hadi sasa hatujapewa taarifa rasmi juu ya kiasi tutakacholipwa. Jambo la kwanza, sio sisi wabunge tunaoamua tulipwe kiasi gani cha mshahara na posho mbali mbali. Kwa mujibu wa Sheria ya Uendeshaji Bunge, ni Rais Kikwete ndiye anayeamua masuala haya, baada ya kushauriwa na Tume ya Utumishi wa Bunge. Sheria ya Mafao ya Viongozi wa Kisiasa imeweka masharti ya kiinua mgongo cha 40% ya mishahara yote. Posho nyingine tunazosikia tutazilipwa zitakuwa zimetokana na Sheria ya Uendeshaji Bunge. Ninafikiri hivyo kwa sababu sijaona taarifa yoyote rasmi juu ya jambo hili. Je, nitazichukua??? Ndiyo!!!! Kwanza, kwa sababu nazihitaji kwa ajili yangu na familia yangu kwa sababu baada ya miaka mitano sina akiba yoyote. Ubunge umenitia umaskini ambao sikuwa nao kabla ya 2010. Hii ni ngumu kuaminika lakini ni kweli kwangu na, ninaamini, kwa wabunge wengi. Sisi wabunge ni mobile ATMs, whether we like it or we don't. Pili, kwa sababu chama changu na wagombea wenzangu wa ubunge na udiwani wanazihitaji. Ni hivi, kwenye uchaguzi uliopita wa vijiji na vitongoji ambako tuliimaliza CCM jimboni kwangu, sehemu kubwa ya gharama nilizibeba mimi na, ninaamini, wabunge wenzangu wa CHADEMA walifanya hivyo majimboni kwao. Ukweli wa Mungu ni kwamba chanzo kikubwa cha fedha za CHADEMA majimboni ni wabunge wa chama. Wagombea udiwani wetu wanatutegemea sisi wabunge tuwezeshe kampeni zao kwa fedha, magari na vifaa mbali mbali vya uenezi wa chama na kampeni. Kwa hiyo, choice yetu ni tuchukue ili tupatie vitendea kazi ya ukombozi, au tuache kuchukua tukose pesa za kutuwezesha kushinda uchaguzi ujao. We are not naive, tutazichukua ili tuzifanyie kazi ya kushindia uchaguzi ujao. Tatu, je tusipozichukua ndio hazitatoka??? Hapana!!! Tusipozichukua bado maCCM watachukua zao na, possibly na zetu pia, na watazitumia kutuchapia kwenye uchaguzi ujao. Kipi ni afadhali, tuzichukue tushindie uchaguzi au tuziache ziliwe na maCCM halafu tuchapwe kwenye uchaguzi??? Kwangu mimi ni afadhali kuzichukua, sijui kwako wewe unayesoma message hii. Nne, je tukizichukua tunakuwa mafisadi sawa na maCCM??? Mimi sidhani hivyo kwa sababu nilizozitoa, sijui wewe umasemaje. Wengi wanafikiri wabunge wana hela sana. Wapo wachache sana wenye hela sana, walio wengi ni madeni matupu!!!! Na hii ni ngumu kuamini lakini mark my words: ni wabunge wachache sana watakaotoka na milioni 100 kati ya hizo tunazosikia tutazilipwa!!! Nyingine zote zitaishia kwenye mabenki!!!! I rest my case. Tafadhali sambaza kwenye magroup mengine unakoendelea mjadala huu. Nimesahau group niliyowaahidi maelezo haya jana usiku...
Wakatabahu. Tundu Lissu.


I actually liked Lissu nilivyokuwa nikimskiliza bungeni wakati niko Tanzania nilikuwa namuona mtu mmoja ambaye anakemea UFISADI na vitu vingine ila baada ya kusoma hii statement aloandika i was very dissapointed and usually huwa sipendi sana kuongelea viongozi separately huwa napenda kuongelea TATIZO na SOLUTION maana ukibaki kukemea tatiz halafu huna solution ni kama unaongea na ukuta and what is the point of doing that??

anasema atachukua hela well ni vyema kasema maana wengi watakaa kimya ila yeye amekiri kuwa atachukua,,
amesema wengi wao wana madeni na kwamba wananchi wanadhani mtu akishakuwa mbunge basi automatically ana hela,,kwanini tusifikirie hivyo wakati kila kukicha mnazidi jiongezea mishahara so what happened to kutumikia wananchi?
kingine ni pale kasema hela nyingi huenda kwenye kampeni na kama alivyosema ilimbidi atumie zake so meaning kwamba nyie kama chama mnategemea hela zitokee wapi??
Campaign always needs money and kama wewe uliona unaweza na unafaa KUTUMIKIA wananchi na kuweza kutumia hela yako kufanya campaign kwanini leo ulalamike wakati uliapa KUTUMIKIA wananchi?
na kusema kwamba ohh tusipozichukua CCM watazichukua so inamaana leo CCM ikisema wanakunya posta je na wewe utakunya posta???
sometimes ni vyema kusimama wewe kama wewe na kusema tuu kuwa nazitaka hizo hela but kutoa sababu zisizo na msingi kwangu mm na wananchi wengi ni kama unatudharau au umewafanya wananchi wajinga,,
Mpaka sasa hivi have you made sure JIMBO lako wana kile ulichowaahidi??
Ni kipi umefanya ukasema I AM WORTHY OF THIS MONEY na sikuongelei wewe tuu bali kila mmoja bungeni alochaguliwa KUMTUMIKIA MWANANCHI,,
Nazihitaji mimi na FAMILIA yangu,,so mtanzania wa kawaida yeye na familia yake na wao hawahitaji ulichowaahidi kama maji,umeme,elimu n.k
NA KUSEMA OHH HIKO KITU NDIO RAIS WA JAMHURI KAAMUA NI KAMA VILE YOU DONT WANNA TAKE RESPONSIBILITY KWA ULICHOKISEMA KUWA NITAZICHUKUA,your words and not mine!!
NADHANI MMESAHAU KWANINI MKO KWENYE HILO JENGO WAKATI KUNA MTANZANIA MPAKA SASA HIVI NA TYPE HAJANYWA HATA KIKOMBE CHA CHAI,,
KUNA BAADHI YA WANANCHI TENA WENGI TU HAWANA ELIMU NA HAWATOKUJA KUPATA ELIMU EITHER SIMPLY BECAUSE MMESAHAU KWANINI MLICHAGULIWA SO UNAJUSTIFY VIPI BY KUSEMA NITAZICHUKUA WITH NO SHAME,,Shame on you!!!
WANAWAKE WANGAPI WANAKUFA KWASABABU YA COMPLICATIONS BAADA YA KUJIFUNGUA?
WATU WANGAPI HAWANA ELIMU BORA LET ALONE KUJUA KUSOMA NA KUANDIKA AMBAYO NI HAKI YA MTANZANIA?
HAKUNA DAWA WALA HOSPITALI NZURI KWA MTANZANIA MWENYE MAISHA YA CHINI NA HATA TAJIRI UNAWEZA KUFA HOSPITALI SIMPLY BECAUSE HAWANA DAWA..
KUNA MDA UNAFIKA KUKAA KIMYA PIA NI BUSARA,,
SIJUI NANI ALIKUSHAURI UTOE HII STATEMENT NI BORA HATA UNGEKAA KIMYA TUU BUT THEN AGAIN THIS IS WHAT IS SO BEAUTIFUL ABOUT HUMANNATURE MAANA UMEONYESHA MAKUCHA YA WENGI MLIOMO BUNGENI,,HONGERA KWA HILO!!
KINGINE NI KWAMBA UMEONYESHA PIA UDHAIFU WAKO WHICH MADE ME REMEMBER KUWA SAYING NO IS THE HARDEST THING NA WEWE HAUKO TAYARI KUFANYA MAAMUZI MAGUMU WHICH ALSO MADE ME THINK OF MY DEAR FRIEND WHO ALWAYS TELLS ME NURU YOU BETTER STAND FOR SOMETHING THAN DIE FOR NOTHING,,NIMEMALIZA.COM NA MTANZANIA PIGA KURA IF YOU WANT TO SEE MABADILIKO,,


1 comment:

Anonymous said...

Nina mambo matatu nataka kuuliza na kuweka hapa
1. Ruzuku wakichukua zinaenda wapi?
2. Kwanini ofisi zao za mikoani ni za kukodisha?
3. Kwanini mambo ambayo awali walipigia kelele, now wao ndio vinara wa kusapoti?
Nina mengi ya kujiuliza na kuandika lakini nataka watanzania wajitambue na kutambua hakuna chama kitakachokuja kukukomboa, utajikomboa mwenyewe, hawa wanasiasa kila mmoja anatafuta tonge kwa rangi yake nzuri ya bendera. Mengine ni mbwembwe tu kama kucheza mziki disco, jiulize walikataa posho ya laki kadhaa wakidai ni ubadhirifu, lakini leo wanachukua mil 230 kwa kauli nyepesi, eti Rais ndio anapitisha, kwani posho anapitisha nani? Hapo hapo anakuambia wanageuzwa ATM, ni rahisi kusema maendeleo hayajafika jimboni ndio maana njaa kali, cdm imepoteza mvuto kwa kiasi kikubwa kuliko nilivyowahi kufikiria. Angalia kwa sasa watu wanavyoandika barua za kuachia nafasi zao na kaondoka, ndio kusema NOT YET UHURU, kwa wale tulitegemea mabadiliko kupitia upinzani tuna miaka 20 ya kujiuliza tena. Inaumiza sana.. Nikipata nafasi nitakutumia makala ya mabadiliko hafifu dhidi ya kiu ya mabadiliko halisi, kama nitapewa nafasi. Nawasilisha