Genuine Nordic Vodka
Tuesday, May 20, 2014
FROM SETH DE JESUS GIOVANNIE A.K.A BIKIRA WA KISUKUMA!!!
Ukioa Mke Mzuuuriiii,kuna raia utawasikia tu,''Wanawake wa vile hawafai kabisa,huwezi kummiliki yule utagongewa tu atakufilisi'',na maneno kadha wa kadha...Kwani Mademu wazuri hawana Hisia au mnadhani mioyo yao inapitisha Utomvu badala ya damu??
Ni kweli kwamba Watu wanaogopa sana kuoa wanawake wazuri kutokana na historia zilizo wazi kwamba 'injini zao za Mapenzi huwa zinanoki bila taarifa na spea hakuna'' lakini Hicho sio Kigezo pia cha wewe Kuoa Kinyago cha Mpapure shangazi yake Sanamu la Michelini ambaye ni mpwa wake Mwajuma Ndalandefu! Utawasikia kisingizio chao,''Mademu wa kawaida ndo Wife Material'',nani kasema??Unaweza ukachukua wa Kawaida na akakumbitsa-kimbitsa kama Usain Bolt ukajuta,Uzuri umekosa na Jalamba unapigishwa kama kawa...Uzuri au Ubaya wa Mtu hauna uhusiano wa Moja kwa moja na U-Waifu matirio
Kimfaacho mtu chake,Oa mtu ambaye wewe na Halmashauri ya Kichwa na Macho yako ya juu na chini yakimuangalia Maruhani yanapanda,Sasa we danganywa ooh oa mke wa kawaida uibuke na Gong'ole halieleweki Boneti iko wapi wala buti iko wapi uone...UNAISHI NAE MILELE HUYO KUMBUKA,Jipatie Chaguo lako ambalo kila akiamka kwenda kuoga unamtazama na Mnara unaanza kuonyesha mawimbi ya kukamata Channel
Msione watu wanasali makanisani kwa Kulia hadi makamasi mkajua wanaombea Nchi yetu isiingie Vitani,au wanaombea Mayatima,Kuna watu wanalia na kulia na Mengi,Wengine wanaomba Wake zao/Waume Zao wafe ili kile kifungo cha Ndoa kitenguke waanze kusagula-sagula upya maana huko ndani wameoana lakini mmoja ameekwa hisia kama Boko Haram
NA mbaya zaidi kadri unavyokomaa Kumuombea Mmeo/Mkeo afe ili ujinasue ndo anazidi kunenepeana na Mashavu yanatoka,HAFI NG'OO,CHAGUA VIZURI KAMA Samuel Sasali,ikifika sa9 anahisi masaa hayaendi akamuone kipusa Milembe John Madaha Ghetto.
Kila nikitaka kuoa NATETEMEKA hadi najisikia kunena kwa lugha Ohhhh rikababababashantarabatarakatashimabataKANTANGAZErikobosikasethkatisharikabosishantahaymah
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
3 comments:
aisee bila shaka huyu mjamaa ni chizi au ana akili nyingi hadi zinamwagika.
ANAONGEAGA UKWELI NA POINT TUUU,,ITS THINGS TUNAVIFIKIRA ILA HATUVIONGLEI BALI YEYE KAGUNDUA NJIA YA KUYAONGELEA AU KUONGEA UKWELI NA POINT IN A WAY KILA MTU ATA RELATE TO IT,,HICHO NI KIPAJI
hahahah nimecheka mpaka nimeumwa mbavu,huyu mtu ana kipaji cha uhandishi,na ni ukweli mtupu.
Post a Comment