Genuine Nordic Vodka

Genuine Nordic Vodka

Thursday, July 27, 2017

WHAT A TRAGEDY,REST IN PEACE NORAH J MAREALLE!!!
Kwanza kabisa poleni sana wazazi kwani ni mtihani mkubwa sana.
Sio mpaka mtoto apoteze maisha ndio muanze kupiga kelele kuhusu sexual predators.
Mapedophile wapo na wengine ni ndugu kabisa au majirani ila watu na jamii bado wanaficha sana hili janga.
Uswahilini watoto wanavyoachiwa ovyo mitaani ni kama mnawasevia mapedophiles chakula mchana kweupe.
Vijijini nio sitaki hata kuimagine.
All in all mbakaji,a pedophile hufanya popote pale as long as kuna mtoto.
Na some family members wanajulikana kabisa kuwa wana hiki kitabia ila bado wanaachiwa jamani mnauwa watoto wenu kwani atakapobakwa hicho kitu kitamuathir mpaka ukubwani.
Huu ukimya unamsaidia nani?
Ukimya huuwa na kuumiza tu na si kingine..
It is high time watu waelimishwe madhara ya kubakwa especially kwa mtoto na kichukuliwe serious.
Nilikuwa naongea jana kuhusu hili naambiwa wengi wanahukumiwa ila bado tatizo ni kubwa sana nikajiuliza source ni nini?
Sometimes mmekalia oh Zari hajalia msibani dafuq....kumbe jirani yako ni shetani muuaji ila utajuaje huku concetration iko kwingine kwani sometimes hawa watu kuwajua si ngumu sana ukifuatilia movement zao na maongezi yao since they cannot help themselves.
Hii ni a very serious issue na tunaweza kuokoa by kuelimishana,kuongea na kutokejeli walioathirika kuwafanya wajione wamekosa kumbe wamekosewa,Nimemaliza.com!
Images by Globalpublishers

3 comments:

Cute Olive said...

Nimeumia sana jamani hivi kweli unyama wote huu sijui nisemeje poleni sana wazazi ndugu na rafiki walioguswa na msiba huu kweli inasikitisha. tunaomba serikali ichukue hatua kali dhidi ya mtuhumiwa mana ni unyama uliopitiliza.

Bintinyota said...

Inauma sana.
Ni jioni hii hii nilikuwa salon kuna Dada anasema anasafiri hivyo inambidi kumpeleka binti yake kijijini kwa bibi yake kwa huo muda hayupo, koz anahofu mwanaye kujafanyiwa vitendo viovu maana mtaa wao umechafuka, na mmoja WA wabakaji anajisifu (ya dogodogo tamu)!!! Yuko mtaani akiwabaka time to time na kuachiwa kiss eti ana cheti cha mental really?

So awamalize wote?
Then Mtoto akipata mimba na shule basi? Kwani ilikuwa ridhaa yake kubakwa?

Ukiwa bado unapumua, usiseme siwezi kudhuru MTU. Ukimkuta MTU anambaka mwanao hujui utachukua hatua gani.

Mungu atustirie vizazi vyetu. Ameen

Mjomba? 11yrs child? SubhannaAllah.
Mungu awape Subra familia.

Irene said...

majanga haswaaa maana hii sasa aibu kama mtu wa karibu kabisa anaweza mfanyia mtoto wake kitendo kama hiki