Genuine Nordic Vodka

Genuine Nordic Vodka

Saturday, July 15, 2017

The Tale About The Masai Warrior!!!


Najiuliza maswalii kadhaa..,

Hivi ni binadamu wa aina gani huamka tu na kuanza kutukana watu bila sababu?
Ni binaadam gani anaona yuko sawa kusambaza chuki hata kwa waliomzidi...
Ni binaadam wa aina gani anapata faraja wakati akisimanga wenzake?
Ni binaadam gani anamtukana mtu anayesema anamchukia lakini kutwa anamfatilia step by step sasa hiyo ni chuki au unatamani kuwa kama yeye..
na kama ni chuki je kifanywe kipi yaishe?
Unaanzaje mfuatilia mtu usiku na mchana unayesema unamchukia na kupoteza mda mwingi kufuatilia maisha yake wakati ukute yeye hana hata time na wewe...
Unajiskiaje pale unapokiponda kitu lakin kila siku unakifuatilia?
Isnt it about time uchukue muda,ukae utafakari na kujiuliza je hii chuki inakupa faida gani?
with everything kuna faida na hasara sasa kama kwako unaona chuki ina faida kuliko hasara then jua kwamba hasara ni wewe mwenyewe.
Chuli ni kitu kibaya sana kwani kinakufanya ufumbe macho hata ukweli uukatae.
Chuki itakupa faraja momentarily ila sio entirely kwani kila siku utakuwa ukimuona huyo huyo unayemchukia akipiga ka step.
Na siku utakayo kuja kujigundua kuwa ulipoteza mda mwingi sana doing useless things utasikitika au utazidisha hasira..
Kama una chuki na mtu kiasi kwamba unamuombea mabaya hata akiongeza nyanya tuu utakereka kwavile ulikuwa unasubiri aanguke sasa swali langu je Mungu kweli atakubariki ikiwa unawaombea wenzako mabaya?
Wote hapa duniani Tunamuomba Mungu mmoja ila Dua na nafsi zenu zinatofautiana.
Sie kila anayetizama juu humuomba Mungu bali wengine humuegemea Shetani,Nimemaliza.com!

4 comments:

Cute Olive said...

Umeongea yote Nuru chuki ni kitu kibaya sana kwanza hata kiafya sio nzuri mana utakuwa unawaza mambaya tu kwa mwenzio ili hali hana habari wewe ndio utaumia zaidi

Anonymous said...

Maswali mazuri ila soma
Emotional person diseases kisha soma walopata matatizo utoton ,wakaish na majuto au mchungu mpk ukubwani."UTAWAJUA WANADAMU UTAPATA NAFASI YA KUWEWEKA KWA MAFUNGU.
KISHA SOMA PSYCHIATRY 1 & 2 PSYCHOLOGY 1.
Ktk psychology utakuta sie binadamu tuko mafung 3
1.mimi
2.yule
3.zaid ya mimi.
Hawa 3 ndo kuna mwenye imani na huruma
Kuna mwenye kisasa na kulipiza
Kuna wenye chuki kuridhisha au kulipiza walopitia.
Ukiwajua hupotezi muda kuwafumbia kuwajibu
Kuumia
Kujiuliz kwa nini?
Mimi binadamu nawatafsiri ktk makundi kama niwajuavyo wanangu .

Anonymous said...

The Light point nzuri sana napenda kusoma vitu kama hivi nakukubali

Irene said...

true my dear haters awahitaji sababu ya kukuchukia and sometimes mna different back ground the way mmeanza maisha mnatofautina and still mtu anakuchukia. huwa najiuliza sanaa nakosa jibu sometimes vyeo tofauti and total different life and still someone is busy searching for your downfall.