Genuine Nordic Vodka

Genuine Nordic Vodka

Tuesday, May 23, 2017

BLACK SOAP!!!Kuna mdada uliniandikia unaweza kupata wapi hii Sabuni Tanzania  Kariakoo maduka ya jumla na Dar Free Market kwenye maduka ya mambo ya urembo na vipodozi hauwezi ukaikosa hii sabuni ila Online unaiweza pia ipata na kuroder.
Binafsi huwa nanunua kutoka Uk au online kwavile Sweden haziruhusiwi madukani.
Uingereza na Usa zimejaa kama uchafu but its because ya wageni ni wengi na kwa wenzetu wa West wamekuwa wakiitumia mda mrefu sana.
Nzuri zaidi ni ile black Soap yenyewe ambayo iko kama udongo but hata hii ni a very good alternative.
Kunna watu hodari huwa wanatengeneza shampoo kwa hii black Soap ntajaribu tizama a video nikipata nitawawekea.
Ni Sabuni nzuri but mwanzoni huwa inakausha kidogo ngozi so usishtuke ila kuwa tu unamoisturize ngozi yako kwa either lotion au mafuta ya asili.
Unaweza itumia mwili mzima hata sehemu za siri na baada ya mda utaona results zake kwani ngozi inakuwa laini kama ya mtoto mdogo.
Usimix ma cream ya kujichubua na hii kitu kwani hizi ni natural ingredients hii Sabuni haina machemichal so pliz stick to one thing and one thing only.
Siri ya ngozi ni kutokutumia ma cream mengi kwa wakati mmoja.
Pombe,Sigara,Usingizi,Stress,Allergy kwa mfano tizama Pia unachokula kwani Pia vyakula wengine vinawafanya u break out na ngozi especially usoni hutuonyesha ni vile tu hujui so chunguza na kukeep track kuna watu hawali chocolate akila tu ni kosa atatoka mapele usoni so kuwa Makini na kipi ambacho kinakudhuru.
Facials Pia ni muhim kufanya kwani ngozi hata utumie nini kama ni chafu hakuna kitachoisaidia.
Jaribu kuupa uso wako time to breathe na sio kuupaka make up kila siku.
Kunywa Maji ni muhim but zingatia yote kwa pamoja and I think all Will be well!

5 comments:

SUZANA ANORD said...

yani asante sana da nuuu kwa hizi tips
mana mie napenda kula vitu vyenye sukari na nahisi ndio vinaletea viepele usoni mana wala sio chunusi
asante sana
nikienda dar nitatafuta hapo dar free market

comfort said...

Nitaitafuta.ila hiyo uloiweka hapo tofaut na ninazoziona huku.sasa sijui ndy feki hizo kwanza ni ndogo hii naiona kubwa na umbo tofauti nilioina huku Pharmacy moja hivi niya pembe nne.

anonymus said...

Hizi zipo kariakoo kwenye maduka ya jumla ya vipodozi.mwamini

NURU THE LIGHT said...

Ahsante mpendwa 10.48

SUZANA ANORD said...

ohhh!!!
asante sana mwamini mana nilikuwa nawaza kuomba gari ya mjomba nikaringishiiieeee na mie dar free market
mana sie wengine tukitembea utazani vifaru wamepita wakiwa wanakimbizwa na mzee wa pori lake (simba)