Majuzi hapa tumeongelea swala la ndoa na wengi wenu mlisema ndoa ina heshima yake.
Nadhan point ambayo huwa hamuelewi ni kwamba Ndoa haiwezi kukupa heshima hata siku moja kama nyie mlioko kwenye ndoa hamtaiheshimu ndoa yenu,irudie hii sentesi×2
Kuna kitu kinaitwa kuwa Mkweli hapa tuna muigizaji maarufu Tontoh Dikeh kutoka Nigeria ambaye imembidi aongee ukweli kuhusu ex husband wake.
Aisee kuna wanaume dunia hii au NISEME binadamu dunia hii hata uwape nini they are just Who they are.
Kwenye Interview kaongelea kuhusu mumewe alivyokuwa akimpiga sana mara kwa mara na siku ya pili humletea pasta amuombee ili asiachwe na Mkewe.
Kaongelea kuhusu wanawake wanaotembea na mumewe mpaka kununuliwa nyumba na vinginevyo on the list mpaka waigizaji wenzake wa kike.
Kaongelea kuhusu yeye kupata magonjwa kama std kwasababu ya mumewe kutembea na wanawake tofauti nje bila kinga.
Kaongelea watoto wa nje kutoka kwa mumewe ambao alikuwa hajui kwani mumewe alimficha.
Hivi mnajua kuwa Yeye ndio anaubeba mzigo kwa ushenzi wa mumewe simply because yeye ndio maarufu na mwanamke.
Wanawake huwa tunabeba mengi imagine mtu yuko na career yake,anajitegemea jamii inampenda akaenda beba mzigo ambao haubebeki no matter what.
Kilichonipa hope ni mke wa kwanza wa zamani wa shenzimume ambaye kasema Tontoh ndio sasa hivi anamsaidia kwavile yeye alishayapitia,nimeipenda hiyo.
Chukua mda utizame interview yake mimi binafsi nimetoa machozi.
Halafu hii mijitu inayojitia mungu mungu na wa dini kumbe nyuma ya pazia ni wa chafu na nafsi zao chafu jamani Mungu huwa hadanganywi hivi huwa hamuogopi?
Nuru mwanangu mwanaume akikupiga mara moja tu achana nae wala usifikirie mara mbili kwani leo ataanza shavu na keshokutwa utatolewa jicho,naam Mama nimekusikia na aliyejaribu au hata kufikiria hato pata nafasi maishani mwangu.
Usiombe ndoa bali omba mke au mume mwema atakayekupenda,atakayekuheshimu,atakayekubebea kuwa faithfull,kutokukupig,kuto kutesa na mtakuwa BEGA kwa BEGA kwenye kila jambo,Nimemaliza.com!
Tonto Dikeh
8 comments:
it is so sad , I have watch full interview kwa kweli wanawake tunapitia mambo mengi sana na magumu , Mungu atupe ujasiri wa kusimamamia familia zetu. I cried for her
Horrible Interviewer how i wish it was Oprah but I do feel for Tonto atleast she was strong enough to get out.
Marriage should be filled with love and respect for each other and your kids no matter how many years you have together.
NURU MAMY NDOA INAHESHIMA NA INATHAMANI KTK NCHI MASIKINI NA ZISIZO ENDELEA.
NANI ALOKUTANA NA MTU MZIMA ANAYEMUHESHIMU NA KUSEMA HUYU BWANA ANGU .
HIVI VYA UHAWARA TUNAVIIGA NCHI ZA WENZETU.
KUMBUKA
MWANAMKE NA MWANAUME WANAHITAJI KUBEMBELEZANA
KUTUNZANA,KUHESHIMIANA NA KUTAMBUANA UMUHIMU WAO.
KAMA MTU HANA HESHIMA HANA HATA AWE HAWARA.
AMINI USIAMIN KILA MTU ANATAMANI SIKU MOJA AWE MKE AU MUME,
AWE MAMA AU BABA.ILA NDÖ HIVYOO
NA KUNA WANAWAKE HAWAJAWAHI HATA KUTAMKIWA "NATAKA NIKUOE" NA HANA KASORO.
SASA MTU KAMA HUYU AKIIZUNGUMZIA NDOA ATAIZUNGUMZIAJE???
UKIOLEWA UNA HAKI ZOTE ZA MSINGI HATA UKIACHIKA UTAZIPATA.
HATA UKITUMIA MUDA UTAPATA HAKI YAKO.
NDOA INAHITAJI UVUMILIVE, UJASIRI,MWANAMKE UWE NA CHAKO,UWE NA UAMUZI,USIYE SEMA BILA YA HUYU MIMI SIWEZIKUISHI.Wanaoteseka ni masikini na wasojua kutafuta na wanao sikiliza starehe.
KUISHI UHAWARA MKO FREE NA HAKUNA HAKI ZA MSINGI NA NDO MAANA
"UHAWARA UNADUMU "KILA MMOJA ANAJUA NIKIMUUZI ATAONDOKA.
UHAWARA TUUUWAACHIE WENYEWE WALOUPITISHA NA KUUHESABU NI SAWA NA NDOA MFN SWEDEN.
WANAWAKE TUNATAKIWA
TUSIKIBALI KUNYANYASIKA
TUSIMAME KWA KUJITUMA.
UKIGOMBA NA AU KUFUKUZWA UNAPOPAKU KIMBILIA.SIO KWENU TENA. TUSIWAPENDE WANAUME MPK UKINYANYASIKA AU .LUKIPIGWA HUTAKI KUONDOKA"KISA PENZI.
ANGALIA NCHI ZILIZOENDELEA ANAYETESEKA NI YULE ALOKUWA TEJA WA MAPENZI TU.ANAMPENDA MWANAUME NA KUKUBALI MATESO.
soma Vålde I nera relationer.
Uktag unda ni mapenzi Mubashara tuu ndo yanasababisha yote.
Watu wanaishi 50% kila kitu
Wako wenye
Socialbidrag
Hakuna kuhongana
Mtu anakazi na mshahara
Hapo ukiteswa si ujue Mhogo ndo umekuchanganya!!
MTZ mwenzangu anafanya kazi nurse .Anaishi na MTZ alomleta.
Mwanamke ndo anakazi na mshahara mzuri.
Ila mwanaume anamtesa anatembea na MTZ kafa Kaoza kwa hawara.
Huyo nurse analazwa mpk allmän psykiatri sasa Nuru hao JIULIZE upate jibu.ninini???
siku hizi bongo wazazi wanajua kabisa wazi kuwa flani na flani are not married na wamezaliana Diamond na Zari mfano tosha,,,
NA kingine usiusemee moyo wa mtu kuna watu hawataki kuowa wala kuolewa eleweni hilo wewe jiongelee wewe kama wewe na heshim maamuzi ya wasiotaka na hilo ndio tatizo wengi wenu mnajiongelea from ur point of view tizameni both sides
Mengine umeongea point nzuri sana umefafanua vizuri mno Nimekupenda bure na huyo Nurse mungu ampe nguvu aamke achane na hilo dume SURUALI dah kwanini kisa tu una bwana jamani tena stori za hivyo ni nyingi huku ulaya huwa sielewi Dah stackars henne .
Uko sawa Anony. ..Lakini huyo mwanaume alishakuwa na mwanamke kabla ya Tonto na hakudumu naye. Ni tabia za baadhi ya weusi .kumtesa mwanamke anayejua anampenda .
Tusi ogopa nyumba kwa ajili ya wanaume washenzi .
Wapo wanaume wenye kujua thamani ya mwanamke bwana. Sio wale wanaomtest mtu kwa ajili.
Asante Ila sijaongelea Moyo wa mtu Nuru mpenzi .
Wanaopenda uhawara ok nilishaupitia kwa kuficha na nnajua pande zote mbili hasara na faida zake ni maamuzi ya mtu.
Inategemea umezaliwa ktk familia gani?
kuna waloishi kimada????
Walozaa nje ya ndoa
Walozaa dini tofauti.
Kuna mila
Malezi
Heshima
Maadili nk.
Kuna mtu anapenda kuvaa nguo fupo ila akivaa anatafuta pakukatiza "Malezi"
Kuna mtu anajiacha uchii na haoni aibu mf Gigy.
Kuna wanaotamani ndoa na hazijawafikia (Mungu awabariki)
NA kuna wa sio tamani pia.
Kuna wanaotamani mtt mpk wanakufuru.Mungu awape japo mmoja)
Mfanyakazi mwenzangu anakwambia hafikirii kuzaa na wala hata mani mtt.
Kuna Pepo /Moto
Machungu /furaha
Kuzima /kufa
Huyo x wa Tonto alishawahi
Kuwa na mwingine miezi na aka mwacha.
Kuna star a natamani awe na star hata akiteseka awe nae tu.
Nilivyosikiliza na nilivyoelewa namuona kabisa Tonto anaumizwa na Penzi. Na ktk moyo alitamani mwanaume angekuwepo perfect.
Ila wanawake wakijitambua esp weusi au tulotoka ktk nchi masikini. Tutatokomeza manyanyaso.
Tutatokomeza mateso bila hivyo mpk vitukuu vyetu vitateseka
Angalia nchi zipi wanawake hawana haki my dear.
Mtu akimpenda mwanaume anamfanyabiashara kama ndo moyo .Useme ukisoma atakufa.
Mie jasiri sikubadili kuteseka au kuteswa hilo nimeliweka mwishö kama kifo.
Na wa elezea wanangu japo wadogo wajikubali wanaweza na kujitambue.
Moyo sukuma damu ..
Nilikuwa off umeniweka busy my dear.
Kila la kheri
mtazamo wangu. Umetoa mfn Mond na Zari . Ukifatilia nyuma utakuta hata wazazi wao au mmoja wao hawaziri ndoa na walifata watoto rangi nyingi.
Huyo nurse Mungu ampe nguvu.
Mimi jamani Allah anisamehe lkn hata my mom nimemwambia siwez vumilia mwanaume aninyanyase eti kuogopa aibu ya kuachika! Hee ninayepata tabu ni Mimi si watu!!!
Nitakipa.
Na Principal yangu ya mwanzo ktk maisha! Cha mwanaume kwangu nyongeza.
I Stand on my Feet!
Ukileta zakuletwa Sepa baba
Anon wa 3.16 aisee umenipa faraja,furaha na kunihamasisha kwani leo umenifunza kuwa nina wasomaji wanajua kutizama pande zote,kuchambua na kutizama kitu kwa kina kirefu ahsante sana my dear maana majuzi yule mburula alokuwa hajaelewa maana ya kumpost will akiwa Tanzania na kuitangaza nchi yetu ghafla nilipata wasiwasi ila umeirudisha imani yangu na Bintinyota wangu pia as always tokea nimeanza 2009,,
Kama mtu mda huu yuko kwenye mahusiano na hana amani akisema koment zenu ATAPATA moja au mwili na akitizama interview atapata mengi,,
Post a Comment