Genuine Nordic Vodka

Genuine Nordic Vodka

Wednesday, February 3, 2016

AND THE SAGA CONTINUES!!!






Chama kikuu cha upinzani Zanzibar CUF, kimeitaka
Tume ya Uchaguzi visiwani humo ZEC kuondoa na
kutotumia karatasi za kupigia kura zenye kuonesha
jina la mgombea wake wa urais pamoja na baraza la
wawakilishi kwa lengo la kugomea uchaguzi wa
marudio uliopangwa kufanyika Machi 20 visiwani
humo.. @Dw kiswahili



Maalim Seif Sharif Hamad anazungumza
na viongozi wa CUF wa Wilaya zote na
Majimbo yote ya Unguja muda huu kwa
lengo la kuwafafanulia Azimio la Baraza
Kuu la Uongozi la Taifa la Chama la
kutoshiriki kile kinachoitwa uchaguzi wa
marudio uliotangazwa na Jecha Salim
Jecha.
Maalim Seif anasisitiza kwamba uchaguzi
ulishafanyika na kukamilika tarehe 25
Oktoba, 2015 na umethibitishwa na
waangalizi wote kuwa ulikuwa uchaguzi
huru na wa haki. Waangalizi hao ni
pamoja na wale wa Jumuiya ya Madola
(The Commonwealth), Umoja wa Ulaya
(European Union), Umoja wa Afrika
(African Union), Jumuiya ya Maendeleo ya
Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC),
Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) pamoja
na waangalizi kutoka nchi za Marekani na
Uingereza.
Anasema kwamba kitendo cha kupindua
maamuzi ya Wazanzibari kupitia uchaguzi
mkuu wa tarehe 25 Oktoba, 2015
kilifanywa kwa baraka zote za aliyekuwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wakati
huo, Jakaya Kikwete. Anasema hakuna
mtu mbaya kwa Zanzibar na Wazanzibari
kama Jakaya Kikwete. Kwa hivyo,
anasema kudai kwamba Rais wa Jamhuri
ya Muungano hana mamlaka kuliingilia
kati suala la Zanzibar ni unafiki wa hali ya
juu.
Maalim Seif ameweka msimamo wa CUF
hadharani kwamba uchaguzi wa marudio
si halali na si ufumbuzi wa mkwamo wa
uchaguzi uliopo huku akisisitiza kwamba
uchaguzi ulishafanyika tarehe 25 Oktoba,
2015.
Amewaeleza kwa kina yaliyojiri katika
vikao 9 vya mazungumzo kati yake na Dk.
Ali Mohamed Shein pamoja na Marais
wastaafu na kuweka wazi kwamba
mazungumzo hayo hayakufanikiwa kwa
sababu Dk. Shein hana nia njema na si
mkweli. Amesema Dk. Shein ni mtu
anayeamini kutawala kwa mabavu na
matumizi ya nguvu na asiyejali wala
kuheshimu Katiba.
Maalim Seif anawataka wana - CUF
kutembea kifua mbele wakijua kwamba
wao ndiyo WASHINDI HALALI wa uchaguzi
mkuu wa Zanzibar.
Amemalizia kwa kusisitiza tena kwamba
msimamo wa CUF kama ulivyotangazwa
na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa UKO
PALE PALE!
Chanzo:Ismail Jussa Fb Account


Katibu Mkuu wa chama cha wananchi CUF visiwani Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, leo amekutana na viongozi wote wa chama hicho wa wilaya za Unguja pamoja na viongozi wote katika majimbo yote 36 na kuwaelezea juu ya msimamo wa baraza kuu la chama hicho kuhusiana na yale yaliyojiri katika mazungumzo ya kutafuta suluhu ya mkwamo wa kisiasa na hatua iliyotangazwa baadaye na mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar-ZEC, Jecha Salim Jecha, ya kurudiwa kwa uchaguzi mkuu kwa upande wa Zanzibar Machi 20!!
SOURCE;DW SWAHILI

No comments: