Genuine Nordic Vodka

Genuine Nordic Vodka

Tuesday, January 12, 2016

WHAT IS THIS!!!!


JE WATU WAKISEMA MANENO HAYA MTAWALAUMU??
Hawa ndio namba moja wa ubaguzi sio wa kidini tu na wa kirangi pia.
Nashangaa hakuna anayelikemea hili.
Hawa vijana waliobeba bango hili siwalaumu sana kwani ni ukosefu wa elimu.

Siasa za. Hatari sana hizi. Siasa za kibaguzi. Siasa zinazopaswa kulaaniwa na kila mpinga ubaguzi nchini. Nitashangaa sana kama wakubwa CCM hamtaomba radhi kwa siasa hizi hizi mbaya kabisa. What will be the stop? by ZITTO KABWE

CCM YAOMBA RADHI
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesikitishwa sana na ujumbe wenye maudhui ya ubaguzi ulioandikwa kwenye moja ya Bango lililobebwa na mmoja wa wananchi waliojitokeza katika maadhimisho ya Sherehe za Miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinaomba radhi kwa ujumbe huo, kinapinga na kinakemea kabisa fikra, hisia na mitazamo yoyote yenye maudhui ya kibaguzi.
Ujumbe huo sio tu kuwa una maudhui ya kibaguzi bali pia unaenda kinyume kabisa na falsafa na Shabaha ya waasisi wa Mapinduzi hayo Matukufu ya mwaka 1964 na unapingana na misingi na itikadi ya CCM inayohimiza Umoja na Mshikamano wa Kitaifa.
Daniel Chongolo
Mkuu wa Mawasiliano na Umma CCM.

12/01/2016


No comments: