Mbunge wa zamani wa Kigoma Kusini, David Kafulila akishuka kwenye Ndege ya Air Tanzania katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es Saalam leo akitokea Kigoma. Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) limefanikiwa kuifufua ndege yake aina ya De-Havilland Dash 8 Q300 baada ya kufanyiwa ukarabati kwenye karakana ya shirika hilo iliyopo jijini Dar es Salaam. Ndege hiyo ambayo imeanza safari zake rasmi leo asubuhi kutoka Dar es Salaam kuelekea mkoani Kigoma na kurejea mchana, ina uwezo wa kubeba abiria 50. Picha na Mpigapicha Wetu #Mwananchi21Januari2016
source;mwananchi
No comments:
Post a Comment