Genuine Nordic Vodka

Genuine Nordic Vodka

Wednesday, December 30, 2015

FROM PAULO MATEMU,TUJIELIMISHE!!!



AFYA... Ujauzito vs Mazoezi
kwa nini mazoezi ni muhiimu sana kwa Mama Mjamzito?
1. Mazoezi husaidia sana kabisa kuboresha mfumo wa damu kutoka kwenye miguu kurudi juu hadi kwenye moyo pale misuli ya mguu inapofanyishwa mazoezi.
2. Mazoezi haya huchangia kupunguza uwezekano wa miguu kuvimba.
3. Mazoezi hupunguza kwa kiasi kikubwa sana cha damu kusimama kwenye haswa pale ambapo mtoto anazidi kukua na kukandamiza mishapa ya damu inayorudisha damu juu. 
4. Mazoezi husaidia damu kuzunguka kwa spidi kubwa zaidi na hivyo kurahisisha kuchujwa kwa takamwili kupitia figo, mapafu, ini na ngozi
5. Kama unafanya kazi za kutulia sehemu moja mfano Bank Teller, basi miguu yako isitulie ichezeshe angalao mara kwa mara, na wakati mwingine chezesha vidole vya miguu. vikunje na vinjooshe mara kwa mara. saa ingine simama fanya kazi, saa ingine kaa endelea na kazi.
Ninatamani Wadada wanielewe katika hili, ili wapende kutembeatembea wakati wa ujauzito.
NB. hakikisha kila siku unatembea angalao kwa muda wa nusu saa. Mwenzi wako akikupa kampani inapendeza zaidi. 



Afya... Sababu za kujifungua kwa operation...
1. Endapo mfupa wa nyonga ni mdogo kuliko ukubwa wa mtoto. 
2. Mtoto kukaa vibaya muda mfupi kabla ya kujifungua. Mtoto anatakiwa atangulize kichwa. Akitanguliza mguu/miguu bado anaweza akazaliwa bila operation.
Ila akitanguliza mgongo au makalio hapo lazima operation. 
3. Mtoto kabla hajaanza kuzaliwa mama anakuwa ameshachoka kusukuma na hawezi tena kusukuma zaidi.
4. Mama ambaye mimba iliyopita alijifungua kwa njia ya operation.
5. Sababu za kitabibu... Mfano Mama akiwa na uvimbe...au cancer kwenye mji wa uzazi njia nzuri kujifungua ni operation.... Au umri mdogo sana au umri mkubwa sana....au imetokea dharura ambayo doctor anaona ni muhimu kufanya operation
6. Mama mjamzito kuchagua.
7. Hata kama utajifungua kwa operation. KUFANYA MAZOEZI NI MUHIMU MNO hasa kea afya ya mama.


Afya: Mwanamke/msichana kupata na Maumivu wakati wa tendo la kufanya ngono
1. Uvimbe kwenye shingo ya uzazi ( hii inaweza kuanbata na dalili zingine mfano kutokwa na damu nda nrefu...au kutokupata mimba kirahisi...au kutokwa damu ata bila kuwa mwezini...maumivu wakati wa period...kuvimbiwa na hata kusikia maumivu kwenye kinena.
NINAMAANISHA maumivu wakat w tendo alafu moja ya hizo dalili hapo juu zikawepo nenda hospital ufanyiwe uchunguzi.
2. Maumivu kutokana na STRESS.... au kuumizwa roho kwa msichana... Kulainika kwa mwanamke kabla ya tendo kunahusisha akili yake na utulivu. Stress humfanya mwanamke akose amani na utulivu wa ndani.... Matokeo yake anaumia. Stress zinaweza kutokana ...mwanaume kutokumuandaa mwenzake...woga....( unasababishwa na mambo mengi sana )
3. Maumivu kutokana na magonjwa...mfano UTI...fungus....herpes..... Maumivu yatokanayo na magonjwa.... Huambatana na moja ya hizi dalili...kutokwa majimaji damu au vitu vyeupe ata kama hufanyi na hupo mwezini...kuwashwa.... Muone daktari
4. Maumivu wakati wa tendo ikiwa mwanamke ashaingia menopause ( yaani haingii tena mwezini ) au endapo msichana hajavunja ungo
5. Maumivu kwa mwanamke aliefanyiwa operesheni siku za karibuni. Hapa ni pamoja na wale waliojifungua muda si mrefu na kuwahi kuanza.
Kama mwanamke hakuongezewa njia na mume ana haraka sana....na mwanamke anajisikia kupona kabisa... Angalao zipite wiki 8 yaani miezi 2.
Na pia mimba ikitungwa nje ya uzazi husababisha maumivu wakat wa tendo. Maumivu haya huendelea hata baada na huzidi ukali kadiri muda unavyoongezeka.

No comments: