Genuine Nordic Vodka

Genuine Nordic Vodka

Thursday, November 12, 2015

SOMO LINAENDELEA,BY PAULO MATEMU!!!



Afya: Malezi ya Mimba. SOMA MPAKA MWISHO.
Kwa vile nchi nyingi duniani clinic ya wajawazito inaanza wakati wa Mimba ina umri wa miezi 5... wadada wengi wanapopata mimba ya kwanza huwa hawajapata elimu ya uzazi. wengine wanapata mimba ya pili au ya tatu lakini wanakuwa hawakuhudhuria clinic ya uzazi kwa sababu mimba hizo ziliharibika kabla ya miezi ya kuuanza clinic hivyo nao hawakupata mafunzo ya elimu ya uzazi.
Wadada mnapokuwa mnatafuta ujauzito, mkifanya tendo la ndoa ikifika siku ya 8 nunua kipimo cha mimba (kinauzwa Tsh 1000 tuu ) pima. ukijua una mimba anza kujitunza na kula vizuri
KAMA UNA MIMBA DALILI HIZI ZIKIPATIKANA NENDA HOSPITAL
1. Kupata kizunguzungu na kichwa kuuma sana.
2. Kupata hedhi, au kutoka damu au kutokwa na vitu kama maji
3. Kupata kifafa, kupata shinikizo la damu au kisukari
4. kuvimba miguu au na mikono,
5. Kusikia moyo unaenda kasi sana au moyo unataka kutoka.
6. Maumivu ya kifua yanayojirudia
7. Kama ushasikia mtoto anacheza halafu, baadae zinapita siku mbili hujamsikia akijigusa au kucheza
8. maumivu ya kwenye nyonga au kinena ( haswa yakiwa maumivu makali )
9. Kama kuna dawa unatumia kila siku, mjulishe daktari mapema wakati unapojua tuu kwamba una ujauzito

Mimba ya wiki 21 mpaka 24
Kwa taarifa yako.... Mtoto katika kipindi hiki ukisikiliza nyimbo laini na yenye mapigo tulivu unaweza ukamsikia anajigusa.
ukiongea nae anasikia, na hapa ndio Wababa wanaanza kupoteza kupendwa na mtoto kuliko mama. sababu zingine nitazitoa ktk siku ya mtoto kuzaliwa...
1. Mama mjamzito anaweza akapata miguu kuvimba. Hii ni kawaida sana na isikuogopeshe.
ILA ukiona umevimba uso gafla, kichwa kuuma, presha kupanda na kutokuona vizuri jaribu kwenda kwa daktari wako /clinic hata kama unajisikia fresh nenda tuu.
Ushauri... penda kukaa umeweka miguu juu ya kitu kama stuli, usisimame sehemu moja muda mrefu. kama lazima usimame basi tembea tembea. vaa soksi ndefu zile zinazobana kama unazo
2. mtoto anakua kwa kasi, anasukuma na kupunguza nafasi ya tumbo/utumbo... hivyo kuvimbiwa au kujisikia kuwa na gesi ni kawaida...
USHAURI....pendelea kunywa maji ya vuguvugu, pendelea kujisaidia (haja zote) kadiri unavyojisikia. usijibane.
3. Mtoto ashakamilika viungo ila anahitaji kukomaa hivyo anahitaji virutubisho. Wengi wa wajawazito kipindi hiki wanakuwa na appetite,
USHAURI... mama mjamzito ale vyakula vyenye virutibisho vyote na ale mara kwa mara kadiri anavyoweza.
TATIZO... wamama wengi wanaogopa kula kwa kuhofia kuongezeka uzito. ni makosa makubwa mno. kula nenepa ukijifungua nyonyesha sana utapungua. ( hata Mke wangu hunenepa sana akiwa mjamzito na hurudi kwenye umodel akianza kunyonyesha )
4. Kukoroma, hii ni kutokana na mabadiliko ya homone kwa kipindi hiki. mwili hujitahidi kuzalisha majimaji ili kuondoa vijimelea vya magonjwa hivyo ndio husababisha kukoroma.
USHAURI. hiyo ni kawaida, na itaisha baada ya muda.
Wataalamu wanasema kipindi hiki Baba anatakiwa kumuonyesha Mke upendo sana.
5. Tumbo kuwa kubwa na mgongo kuuma ni jambo sasa la kawaida na hata kibyongo huweza kutokea. wamama wengine huanza kutembea kwa kutanguliza tumbo mbele.
Tatizo... wanaume na wadada ambao hawajapata ujauzito hufikiri kwamba mjamzito ameamua kuletwa swag... HAPANA... hali anayokuwa anajisikia nayo anaeweza kuielewa ni mama ambaye amewahi kuwa mjamzito tuu. wengine huona ni swag!!!
6. Wababa hufanya kosa la kubwa kipindi hiki.... hupoteza ushirikiano na wake zao.... hii humfanya Mmama mjamzito ajichukie na awe na hasira mara kwa mara, wakati mwingine mama mjamzito anatamani Mume aibebe hiyo mimba kwa siku siku moja tuu ili ajue maumivu yake...
TATIZO... Mama mjamzito anapokasirika....mwili wake hujiandaa ktk hali ya kutaka kumbana,... na hii humuathiri mtoto...kwa wakati huo na baadae.
7. DALILI YEYOTE katika hizi nenda hospital... kutokwa na majimaji, au damu, kuanguka kifafa, kichwa kuuma sana, kupatwa na kizunguzungu, presha kupanda, au mtoto kutokucheza kwa siku 2 mfululizo.
usisahau kufanya mazoezi na kula vizuri na kudumisha usafi wa nguo na mwili. mnataka niwatag... nitawainbox
NB. UJAUZITO SIO UGONJWA. 

Mimba wiki ya 25 hadi 28
Kwa Taarifa yako, kipindi hiki mtoto anaota nywele, NA nywele za Mama zinakua kwa kasi sana kipindi hiki, lakini bahati mbaya akishajifungua hukatika kwa baadhi ya wamama. ( sio ugonjwa )
mtoto kwa sasa anaweza akakojoa.
NB mtoto anakua kwa kasi na mama anajikuta anatamani kula mara kwa mara.
WABABA... kipindi hiki ni kizuri sana kucheza na wake zenu, kuongea na mtoto, na kumburudisha mkeo kwa namna mbalimbali. mtoto anasikia sauti. wababa kuuchez ana wake zao kipindi hiki inasaidia wamama kujisikia vizuri sana na kuwapunguzia maumivu na stress.
1. Wamama wanakuwa wanashauriwa kunywa vimininika vya asili kiasi kidogo lakini mara kwa mara, kwa sababu ni muhimu kwa mwili wake na wa mtoto pia. maji yanampunguzia uwezekano wa ngozi kukauka, kupumua kwa shida au kuhisi kizunguzungu kwa Mama.
Tatizo... Kuwashwa sana na ngozi na kujikuna sana unashauri umuone Daktari
2. Mama mjamzito kipindi hiki na baadae anashauriwa asilale kwa mgongo au kwa tumbo.
3. niliyoelezea jana kama kuvimbiwa, mgongo kuuma, mbavu kuuuma, tumbo kujaa gesi, kuchoka, na namna ya kufanya nimeelezea post za jana na juzi.
4. Mama afanye mazoezi sana, inasaidia kuimarisha mzunguko wa damu kwenye mwili wa mama na kwenye mwili wa mtoto pia.
5. Kadiri mtoto anavyokua na kusukuma viungo vya ndani juu... Mama mjamzito anaweza akajisikia kupumulia juu juu... hii ni kawaida ila akiona amezidiwa aende hospital.
7. Kukojoa mara kwa mara, miguu kuuma, kukosa usingizi ni mambo ya kawaida sana kwa kipindi hiki.
8. dalili za hatari ni zile zile... kutoka damu, kutokwa maji, kuwashwa sana ngozi, kuona kizunguzungu, kupata kifafa, kupawa na presha, kisukari au kuanguka ghafla.
nyongeza... kwa suala la dharura mtoto akizaliwa kuanzia wiki 27 katika hospital nzuri ANAWEZA AKAPONA na kuishi. 

No comments: