Genuine Nordic Vodka

Genuine Nordic Vodka

Thursday, November 26, 2015

PAULO MATEMU AKIENDELEA KUTUELIMISHA JUU YA UJAUZITO!!!




Afya.. Mimba wiki ya 38 - 40 sehem ya 3.
UCHUNGU...na mambo yahusiano na uchungu ( najibu pia swali inbox )
1. Uchungu ni kukakamaa kwa msuli ya ndani ya nyonga na misuli ya nyumba ya uzali, kwa lengo la kusuma mtoto (ili azaliwe.)
1. b. Uchungu husababishwa na kuzalishwa kwa homon na hii hufanya misuli ikakamae.
1. c. Homon hiyo ndio ile pia mnasikia Mama amechomwa sindano ya uchungu. ( sindano hiyo haina madhara kwa mtoto au mama )
2. hatua hii huanza taratibu, hii huchukua masaa angalao 8 kwa Mama ambaye hajawahi kujifungua na huchukua masaa 5 kwa ambae amewahi kujifungua, na huyu wakat mwingine huona hatua hii kama kawaida kwa sababu ule uchungu halisi ni mkubwa.
3. Uchungu hatua ya pili, ndio wamama wengi wanaanza kuusikia kweli kweli,
4. huwamaumivu yake hujitokeza kwa dakika 2 au 3 na hupotea na hurudi tena.
kwa Mama mpya hatua hii huchukua masaa 5 na mama mzoezu huchukua masaa 2...
5. Hatua inayofata maumivu huwa makali, na mara kwa mara zaidi, na hapo njia huwa mengine YOTE yanafata.
KINACHOSABABISHA MATATIZO
1. wamama wengi tangu wiki ya 30 huwa wanasikia maumivu na hufikia mahali wanakuwa sugu na yakianza maumivu ya mwanzo yaani kipengele cha 2 hapo juu, Mama anakuwa anachukulia kama ni yale yale ya kawaida
2. Wamama wazoefu kipindi maumivu yameshika kasi, kwa sababu mbalimbali huweza kuvuta muda... katika kuvuta muda hujikuta wameingia kwenye hatua ya 3 (soma 3 juu) bila kujijua.
na madhara ya hili, wengine hukimbia hospital, chupa ishapasuka... au wanafika hospital bado haijapasuka lakini wamefikia hatua ya kujifungua.
NB hatua ya 3 inahitaji uangalizi wa mkunga muda wote, sasa mama wengine hufikia hatua hii wakati hawajafika hata hospital...
kinachotokea akifika hospital katika pukukushani ndio hapa unasikia mtu alijifungulia koridoni... kwenye gari... SABABU kubwa ni kuwa hospital akifika lazima taarifa muhimu ziingie kwenye mafaili ndio apangiwe kuenda kunakostahili.
WENZETU hufika hospital katika hatua ya kwanza tuu ( yaani 2 hapo juu)
3. wamama wengine husahau tarehe halisi aliyopata mimba
hivyo hajui tarehe tarajiwa.
NB wamama wengine ambao unasikia wanafika hospital wakajifungua ndani ya masaa 2, ujue huyu ni jasiri na alifika hospital alishachelewa.
USHAURI....
a. Mama mjamzito akishafikisha wiki ya 37 na kuendelea akipata maumivu ya uchungu anashauriwa aende clinic au hospital husika.
b. Mama akiona chupa imepasuka aite tex au bajaj awahi hospital hata kama wiki gani.
c. mama akiona ameanza kusikia maumivu madogo na anasikia mtoto anasukuma chini aende hospital au clinic aliyopangia kujifungua.
MADHARA YA KUUCHELEWA kwenda hospital ni
pamoja na mtoto kuchoka... na mtoto anaweza akazaliwa ana matatizo yatokanayo na kuuchelewa kulia (soma status ya juzi)
pia chupa kupasuka ni hatari kiasi kwa mtoto endapo atakosa msaada wa mtaalamu
AJABU NA KWELI.... Mpaka leo wanasayansi wamejitahidi kutafuta CHANZO cha uchungu, yaani ni nini haswa kinauambia mwili kwamba sasa uchungu uanze. japokuwa bado watafiti wanaendelea na kutafuta jibu....
MIM hapa ndio ninakoona kama kuna MUNGU ( ALLAH )
maana hakuna anaejua pia kwa nini mtoto anakuwa ananyonya kidole akiwa tumboni... kwa nini mtoto anaanza kunyonya!!! ni nini kinamfanya ajue kwamba maziwa yatatoka....
kuna siku wanasayansi watapata jibu lakini bado kuna NGUVU YA ASILI inafanya kazi... ukiita hiyo nguvu ni MUNGU ( ALLAH ) sitapingana na wewe.

No comments: