Yericko Nyerere 19:34 Today
Ndugu zangu poleni na mapambano,
Kwamda wa mwezi mmoja na nusu sasa nilipotea mitandaoni na katika majukumu mengine ya kimageuzi.
Laa hasha, sikupotea kwa maana ya kuyasaliti mapambano ya ukombozi wa Tanzania, mimi ni mtu huru sawa na matakwa ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Uhuru wangu huu unaotambuliwa na katiba ya nchi, umepokwa na maadui wa ukombozi waliochini ya mwavuli wa kisiasa.
Ndugu Watanzania, Taifa linaingia katika uchaguzi mkuu siku tatu zijazo yaani jumapili, Kwaajili ya kulinda Amani na Umoja wetu unaopita kwenye jiwe la moto, nisieleze UNDANI wa yaliyonisibu na WASIBUAJI katika siku 45 ngumu kabisa tangu niwepo duniani, nikipindi ambacho nilikuwa naupigania UHAI wangu pande zote yaani angani, majini na nchi kavu.
Nawaomba watanzania msiogope, kuweni majasiri wakulinda haki zenu za kikatiba na kutii sheria za nchini na sio vinywa vya kisiasa, kwa umoja wetu, tujitokeze kupiga kura kwa wingi na kura hiyo tumpigie Mh Edward Ngoyayi Lowassa aongoze mabadiliko kutoka kuwa taifa la kikundi kidogo cha kihalifu kiitwacho ccm kinachoendesha uhalifu nchini kwakulindwa na baadhi ya vyombo vya dola.
Ndugu zangu, nataka mfahamu kuwa ccm imehama kutoka kuwa chama cha siasa na kuwa genge la uhalifu nchini linalobaka matakwa ya umma kwamsaada wa vyombo vya dola, hakuna njia ya mkato ya kuitoa ccm madarakani bali ni kupiga kura kwa wingi na KUZILINDA kura hizo kwamjibu kwa katiba na sheria za tume ya uchaguzi na sio huruma ya wahalifu hawa wanaowalazimisha tukalale baada ya kupiga kura.
Dhambi kubwa ambayo hata Mungu hatatusamehe ni kitendo cha sisi kupiga kura na kurudi majumbani mwetu kulala na kuacha wahalifu hawa watuhesabie kura.
Sisi wanaukombozi tuliombele ya mstari wa vita hii tumeshamaliza kazi kwa asilimia miamoja, hatua iliyosalia ni ya watanzania wote kulinda kura zetu mpaka Mh Lowassa na wabunge na madiwani wa UKAWA watangazwe wameshinda ndipo tutembee vifua mbele maatako nyuma tukiusherekea uhuru wetu wa pili.
Niwahakikishie mimi nipo nimzima wa afya, Mungu hakutaka yatokee waliyokusudia watesi na wanyang' anyi wetu.
Natumia fursa hii kuwakumbusha ccm, jeshi la polisi na vyombo vingine vya ulinzi na usalama, UHAI wa binadamu hauishii kulindwa na katiba ya Tanzania wanayoifinyanga tu bali Uhai wa binadamu unalindwa na Katiba ya ULIMWENGU! Tanzania ni yawatanzania, matakwa ya umma yaheshimiwe, Wasiipendelee UKAWA wala wasiipendelee ccm, Bali wawapendelee Watanzania tu.
Sisi wanaukombozi tunaipigania Tanzania ambayo nyinyi vyombo vya usalama mtaiishi kesho, tunapigania ili kuboresha maslahi ya askari wa Tanzania, Tunapigania ili mtoto wa askari huyu asome bure kuanzia chekechea hadi chuo kikuu, tunapigania ili familia za askari hawa zitibiwe bure na huduma nyinginezo nyingi. Hatupiganii matumbo yetu bali ndoto za Watanzania wote.
Natoa shukrani za pekee kwa Mwenyekiti wa Chadema Mh Mbowe na Familia ya Mheshimiwa Lowassa ambao wamesimama nami katika kipindi chote kigumu, pia niwashukuru makamanda na marafiki zangu mitandaoni ambao kwahakika ninalo deni kubwa la kuwalipa kuanzia jumapili.
Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki UKAWA
No comments:
Post a Comment