Watu hawa(Tarime) pia wamechafuka sana kwa maji ya mgodi na asili ya udongo mwekundu, afya ziko mashakani, chakula hakitoshi kwa sababu watu wanashinda migodini kutafuta mchanga.
Ni halali kweli kuwaacha watu wa Tarime bila dalili zozote kuwa dhahabu yao ina thamani kwao pia?
Tukipita barabarani tumekutana na makundi ya watoto, vijana, wanawake na wanaume wanaotoka kuchuja mchanga kwenye maji nje ya eneo la mgodi. Unaanza kuuona umasikini wa tarime hapo, unaona nyuso za watu zilizochoka na kukata tamaa. Unaona kiu, njaa, maradhi, kuachwa na kukosa utetezi.Tarime ni moja ya eneo nisingetegemea kukuta umasikini wa kuzidi. Mgodi wa madini umewaacha wananchi wakihangaika na mchanga kutafuta masalia ya vipande vidogo sana vya madini.
No comments:
Post a Comment