Honestly sioni tatizo kwa wasanii kutumiwa na wanasiasa kwenye kampeni zao kama ambavyo tunashuhudia sasa na hiki sio kitu kipya. Tofauti ya miaka mitano iliyopita na sasa ni kuwa uchaguzi huu umekuja katika kipindi ambacho matumizi ya mitandao ya kijamii yamepamba moto. Wanasiasa wanawatumia wasanii si tu katika kuwalipa na kupanda jukwaani kutumbuiza bali wanawataka pia watumie akaunti zao za mitandao ya kijamii kupenyeza propaganda zao – na hapo ndipo tatizo lilipo!
Zamani enzi akina Marlow wanashiriki kwenye kampeni walikuwa wanapanda jukwaani wanafanya yao, wanawaburudisha mashabiki wa chama husika na kila mmoja anaondoka yuko happy! Hakukuwa na masuala ya social networks wala nini! Leo hii tunashuhudia jinsi inavyoleta ukakasi kuona post za mastaa zikilazimisha followers wao waamini katika mrengo waliomo wao na actually si kwa kupenda tu, bali kwasababu wamelipwa!
Muktadha huu ni tofauti hapa kwasababu msanii ana followers wenye itikadi tofauti, wapo wanaomuunga mkono na wapo wanaokerwa! Tukumbuke kuwa uhusiano kati ya msanii na shabiki ni kuhusu muziki pekee! No wonder wengi wanatukanwa sana!
Again, si mbaya wao kupost kuhusu interest zao lakini wanakosea sana pale nao wanapoanza kuandika propaganda na kuuponda upande wa pili! Hiyo ni kazi ya mwanasiasa, si kazi ya msanii! Mwache wanasiasa mwenyewe aingie kwenye vita hivyo, wewe kama msanii nenda jukwaani katumbuize mashabiki wa chama hicho, then sepa! Usianze kuponda na kutukuna wanasiasa wa upande wa pili kama vile na wewe unagombea!
Tunachokiona sasa kina madhara makubwa katika uhusiano kati ya msanii na shabiki! Wasanii kuweni makini! Na hii inawahusu wasanii wote walio kwenye mirengo walioichagua!
Mungu ibariki Tanzania na zifanye kampeni ziwe za amani by @skytanzania

No comments:
Post a Comment