Naitwa Aziz, mmiliki wa Aziz house if jeans Kariakoo.Nilianza biashara mwaka 2008 nikiwa nauza tops za wadada na baadae nikaanza kuuza jeans.Wakati naanza niilianza na jeans saba 7 tu ambazo nilikuwa nanunua hapa hapa kariakoo.Nilikuwa nikiuza na kurudisha pesa kwa mali kauli.Nilikusanya pesa kidogo kidogo baadae nikipata mtaji ilipofika 2010 nikaanza kwenda china.Na wakati naanza kwenda china nilikuwa nina mtaji wa tsh Ml 10 tu.Tayari nilishajiridhisha na kuona biashara ya jeans naiweza na pia ina wateja.Vazi la jeans haliishi fashion lipo tu na linapendwa.Nikaanza kuleta kuanzia hapo 2010 mpaka sasa 2015.
MAENDELEO
kwa sasa nashusha mzigo kila mwezi.Nikishusha mzigo nauza jeans moja 15,000 na baada ya mwezi tunafanya clear sale ya tsh 10,000.
Kwa sasa naweza huza kwa siku jeans zaidi ya laki 2 hasa siku ninazofungua mzigo.
CHANGAMOTO
changamoto kwa kweli hakuna na pia nashauri watu wasiogope biashara kila kitu kinaanza na udogo mpaka kikubwa.
MAFANIKIO
Mimi namshukuru mola sijaogopa kuanza,tena nilianza kaa udogo sana.
Namshukuru mola biashara imenifikisha mbali na mafanikio yapo makubwa tu.
Pia napenda kuwafahamisha wateja wangu naongeza branch ingine mjini posta.Naanzisha huduma ya mzigo kumfikia mteja pale alipo na nitaanza na wateja wa dar es salaam kufuatiwa na mikoani!
SIRI YA USHINDI
siri ya mafanikio ni kuleta vitu vizuri na kuongea na wateja vizuri na kuhakikisha kila mteja akitoka dukani anaenda kuleta mwenzake au kutoa sifa nzuri ya ( aziz house of jeans)hiyo ndo siri ya mafanikio kwa kweli watu wasiogope kufanya biashara kila kitu ni kujaribu tu.Duka langu liko karikaoo mtaa wa shwahili/mkunguni.
0714637394,0655637394,0767
kwa instagram napatika kwa Accont 2
@Azizi_houseofjeans
@house_jeans
#beinspired
1 comment:
AAAISEE HUYU KAKA ANAKAURI NZURI,UUUWI SINUNUI JEANS POPOTE PALE ZAIDI YA KWA HUYU KAKA.
WE LOVES YOU AZIZ
Post a Comment