Mke wangu mpenzi ni rafiki yangu wa maisha, leo tuna miaka 22 ya ndoa...
Ndugu zangu,
Leo Juni 19 ni miaka 22 tangu mpenzi wangu na mimi tufunge ndoa. Tumekuwa sasa ni zaidi ya wapenzi, ni marafiki wa maisha.
Mwaka juzi pale ukumbi wa makumbusho ya taifa, wakati nikizindua kijitabu kidogo nilichokiandika kumhusu Mzee wetu Madiba, niliwasimulia, na ilikuwa ni mara ya kwanza kwenye public, waliokuwa wakinisikiliza juu ya tulivyokutana mimi na mpenzi wangu.
Nairudia hapa simulizi ile;
Ndugu zangu,
Harakati za Ukombozi ndizo zilizochangia nikutane na mke wangu mpenzi, mama wa Makamanda wangu.
Mwezi kama huu, mwaka 1987 nilikutana kwa mara ya kwanza na mpenzi wangu. Alikuwa miongoni mwa wanafunzi wanne waliokuja Tanzania kwa minajili ya kutembelea kambi za Wapigania Uhuru wa ANC kule Mazimbu.
Katika kundi lao nilimfahamu kijana Bengt Beckstrom. Huyu alikuwa pen pal wangu na tulibadilishana mengi juu ya michezo na siasa. Nilikuwa ndio kwanza nimemaliza Form Four pale Tambaza.
Katika mawasiliano yetu, Bengt akanitaarifu kuniomba wafikie nyumbani kwetu Kinondoni Biafra wakiwa Tanzania. Kwamba walishafanya mawasiliano na ANC, Stockholm na kupewa kibali cha kutembelea Mazimbu, Morogoro.
Na enzi hizo nchi yetu ilikuwa na mfumo madhubuti wa kiulinzi ' Total Defence'- Kwa maana ya ulinzi wa jumla. Ikumbukwe, kama nchi, tulikuwa na maadui wengi.(
Basi, nikawaonyesha wazazi wangu ombi la rafiki yangu, na Mjumbe wa Nyumba Kumi naye akapewa taarifa. Najua hata watu wa usalama walifuatilia ugeni ule wa Kinondoni Biafra na kujiridhisha bila hata wageni kujua.
Hivyo, Kijana Bengt akaja nchini akiwa ameongozana na wanafunzi wenzake watatu. Wote wasichana, na mmoja wao ni mrembo niliye naye mpaka sasa.
Wakiwa Dar, wageni wangu waliniomba niwasaidie taratibu za kuwafikisha na kuwatambulisha kwenye moja ya ofisi za ANC, Dar. Asubuhi moja nikaenda nao hadi pale kona ya Nkrumah Street na Nyerere Road eneo la Kidongo Chekundu. Hapo kulikuwa na ofisi tatu za wapigania ukombozi zilizokuwa jirani; Frelimo, Swapo na ANC.
Nakumbuka kusisimka sana nilipokuwa ndani ya ofisi za ANC na kuongea nao juu ya mipango ya safari ya Mazimbu. Usafiri ulikuwa wa Volkswagon Combi.
Mwaka ule wa 1987 tulikutana na mpenzi wangu kama marafiki tu. Akarudi tena Tanzania miaka miwili baadae, na tangu hapo tupo pamoja mpaka hii leo, na Makamanda pia wamejitokeza!
Hii pia ni historia yangu.
Maggid Mjengwa,

MAGGID MJENGWA WITH HIS FAMILY,,
1 comment:
Gratis sana kaka. Mungu awajalie muishi miaka mia zaidi.
Post a Comment