Genuine Nordic Vodka

Genuine Nordic Vodka

Monday, June 29, 2015

A TRUE STORY,THANK YOU LA PRINCESSA!!!



Siku moja mida ya jioni nilikuwa na haraka sana katika pita pita zangu mtaani kwetu, gari spid kama ambulance sijali hiki wala kile, kumbe mbele yangu kuna gari nyingine nayo spidi kama yangu au zaidi, alikuwa anaingia mtaa niliopo mimi natoka, bahati mbaya akanigonga ubavuni nikasikia kishindo na gari yangu ikazima hapo hapo. Watu wakajazana kutuzunguka na mi nikatoka nje kuliangalia gari yangu. 
Yule mama alitoka kwenye gari ake na hasira, huku akionekana kalewa chakari…akanitukana matusi sijawahi tukanwa tangu nimezaliwa. Niliitwa majina ya kila aina na watu wakimbeza kwamba kosa lilikuwa lakwangu nilikaa upande sio wangu wa barabara. Boda Boda wapambe wote wananisema huku wengine wakimueleze aite traffic tupime kabisaa nimlipe nisijekimbia. Sikutia neno wala kujibu kwani nikaona hamna maana kutukanana barabarani, basi nikanyamaza kimya tangu nimetoka kwenye gari mpaka nimemaliza kutukanwa nikarudi zangu kwenye gai nikachukua simu na maji ya kunywa nikaenda kukaa pembeni kulikuwa maframe ya duka. Yule mama hasira zikampanda zaidi akaanza kupiga kelele kwamba nina dharau na nirudi pale tuongeee ila kwa kweli nilikuwa sina cha kusema na nahisi Kiswahili changu chooote kiliiisha maana hata maneno yalikuwa hayatoki mdomoni, basi nikaa nikinywa maji huku nikimpigia fundi wangu wa gari ambae anaishi maeneo ya pale, nikamsisitiza aje haraka maaana jamaa anaoneka kama anataka kuuleta fujo. Sikutaka kuita polisi wala traffic hata kama kituo kilikua karibu sana na eneo la ajali maana kwa kumuangalia niliona tu Yule mama alikuwa amelewa angewekwa lockup hapo hapo. Baada ya lisaa la kumsubiri Ayubu huyo fundi wangu wapambe boda boda waliondoka na Yule mama akatoa huko alipo akaja pole pole akakaa pembeni yangu 
‘Najua me ndo nimekugonga’
‘Najua’
‘samahani kwa kukutana’
‘Bila samahani ni kawaida barabarani’
‘sasa unamsubiri nani’
‘Fundi wangu anakuja anitengenezee gari yangu niondoke’
‘ila ulikuwa spidi mno’
‘na wewe umelewa’
‘samahani
‘kuwa na amani’
Ukimya ulijaaa wa takribani nusu saa hatukuongea neno…
‘Mme wangu ameniacha… na watoto kaondoka nao kaacha mlango geti wazi, niliipigiwa simu na majirani mchana kwamba nyumba haina mtu na wakaona majambazi wameingia wameondoka na kila kitu kilichokuwemo ndani. Na jana nilitoa pesa zangu zote benki nikaweka nyumbaani, kwahiyo nimechanganyikiwa ndo nillikuwa nawahi kwangu boko’
Machozi yalikuwa yanamtoka huku akiraibu kuyaficha kwa kuangalia pembeni
‘ nilishindwa hata cha kufanya maaana nilifika mwenge nikakutana na foleni nikaanza kunywa viroba tu maana kama ni kuiba wameshaiba, kama ni kuondoka ameshaondoka’
Alilia kwa uchungu karibia dakika ishirini. Sikua na cha kumwambia 
Akafuta machozi yake aakaniangalia kisha akaniuliza kwa upole ‘ wewe ulikuwa unawahi wapi?’
‘ Kuna happy hour hapo Amsterdam pub..shots elfu moja’
Tukajikuta wote tunaangua kicheko
Ayubu fundi wangu akaja akasaidiana na Yule mama kuwasha gari yangu, hatukudaiana
‘Bado unaenda Amsterdam?’ aliuliza kwa upole 
‘Ndio, twende’
Tulienda tukapiga shots mpaka happy hour ilivyoisha kila mtu akaondoka zake. Kesho yake nikakutana nae kwenye mkutano wa mauzo ya hisa ya benki flani mjini. Yeye ndie alikuwa Mkurugenzi, akaniita akanipa tangazo kwaajili ya hayo mauzo nipeleke redioni kwangu, nikamshukuru..mpaka leo ni mteja mzuri sana.
Umejifunza nini?


3 comments:

Anonymous said...

-hii history nimeipenda sana hapa nimejifunza kitu,usilipe baya kwa baya bali lipa baya kwea jema big up, uliyeleta hii story Nuru endelea kuweka story kama hizi tunajifunza mengi asante

NURU THE LIGHT said...



huwa naweka story from time to time especially zenye funzo na nadhan muda umefika tuwe tunastory za maisha au tukio ambalo linatoa elimu kama hii story inavyotoa,,kuna vitu vingi sana kutoka kwenye hii story alone,,karibu mdau

Anonymous said...

Story nzuri sana dada nuru na pia mi huwa napendelea kuangalia blog yako.