Genuine Nordic Vodka

Wednesday, May 13, 2015
UKISTAAJABU YA MUSA!!!
Mwanamume mmoja amecharazwa viboko hadharani leo na waombolezaji wakati wa mazishi ya mtoto wake aliyefariki dunia kwa kile kilichoelezwa kuwa ni uzembe wa kushindwa kumuhudumia. Waombolezaji waliohudhuria mazishi ya mtoto huyo wa miaka mitano yaliyofanyika katika kata ya mkimbizi iliyopo pembezoni mwa mji wa iringa walifikia uamuzi wa kumchapa viboko hadharani baba wa mtoto baada ya kubaini kuwa kifo cha mwanaye kilisababishwa na mwanamume huyo kutoihudumia familia yake. Kisa hicho cha nadra na cha kusisimua kimejiri katika makaburi ya mkimbizi muda mfupi baada ya kufanyika kwa maziko ya mtoto huyo wa makamo. Mwanamume huyo aliyetambuliwa kwa jina moja la Issa alilazimishwa kulala juu ya kaburi la mtoto wake na kisha kucharazwa mikwaju hadi mitano kwa uzembe uliotokana na kuendekeza unywaji chakari wa pombe na kuitelekeza familia kwa kutoipatia huduma. Wakati wa zoezi hilo la adhabu viboko vijana barobaro walimkamata kwa nguvu mzee huyo kiasi ya kushindwa kufurukuta wakati mikwaju ilipokuwa ikimwangukia. Una maoni gani?
Chanzo;Ebony Fm Radio!!!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
3 comments:
kwikwikwikwi.. wamuongeze mbili zangu
hahahahahahah na mm tatu ziwe tano shenzi kabisa
Charaza kabisa, tena iwekwe adhabu kabisa Kisheria wacharazwe wababa wanaokimbia majukumu yao. Hahaaa natamani ningekuwepo na miye ningemtandika zangu mfyuu.
Post a Comment