Bwana Tim S. Grover ameandika kitabu cha ‘RELENTLESS: FROM GOOD TO GREAT TO UNSTOPPABLE’.
1.Usitumie nguvu nyingi kupamabana na adui yako, bali tafuta udhaifu wake kumshinda.
2. Unaweza kukabiliana na hali yoyote ngumu endapo utatanguliza utulivu wa kiakili, na ustahimilivu.
3.Huwezi kuwa mshindi(kufanikiwa) kwa kufuata kila kitu kinachosemwa na makundi au kundi la watu, bali kwa kufanya jambo bora zaidi kuliko yeyote miongoni mwa watu. Na utathibitisha kwanini wewe ni bora zaidi kuliko wao.
3. Unatakiwa kupanga malengo, kutekeleza, kuyaongoza kwa juhudi zako kabla ya kushirikisha wengine.
4.Fanya kazi yako kwa ufasaha. Usiruhusu presha yoyote kuathiri kazi yako maana matunda mazuri yatakupa heshima kubwa.
5.Kama unataka kufanikiwa uanapaswa kujitoa sadaka bila woga. Unaweza kuchukua jambo lolote lenye mtazamo hasi mbele ya jamii na kuliweka kwenye mtazamo chanya.
6.Vita kubwa ya kufanikiwa inabidi upambane ndani mwako kwanza na kujijenga, ili wapinzani wako wakikabiliana na wewe waone ni mshindani thabiti.
7. Usiwe mwepesi kuudhika mbele ya mshindani wako.
8. Usitumie muda mrefu kufikiri bali tumia fanya vitendo.'
9.Unatakiwa kupambana hadi tone la mwisho. Sababu tone la mwisho ni ushindi wako.
10.Imarisha afya yako. Kuwa imara kila wakati ili mwili usivamiwe na magonjwa(fanya mazoezi).
©Markus Mpangala aka Andunje wa Fikra, nimejifunza. Ok nishachoka, weita naomba Azam Juice kidogoooooooo!
No comments:
Post a Comment