Genuine Nordic Vodka

Genuine Nordic Vodka

Monday, May 25, 2015

LUCA NEGHESTI SAID!!!

Kupitia Tuzo za Watu za mwaka huu nimejifunza jambo la kusikitisha kwa kiasi chake, kwamba wanadar es salaam wengi tunaamini kuwa nchi yoooote ipo ndani ya mkoa wetu. Tukitoka nje ya Dar hamna kitu. Wakati hali halisi ni kwamba Dar es Salaam tupo watu milioni 5 kasoro, asilimia 10 tu ya watanzania waishio nchini. Kinachonisikitisha hapo haihusiani na Tuzo za Watu, tatizo ni kubwa zaidi. Mawazo kama hayo yanatupeleka kutothamini utajiri tulionao mkoani, na kuzuia maendeleo ya sekta mbali mbali kama utalii na uwekezaji wa ndani. Binafsi sijatembelea nchi nzima, sijapanda mlima wa Kilimanjaro na bado sijafika mbugani Serengeti. Lakini yale maeneo machache nilioyatembelea sikukosa kuona fursa, na pale nilipokuwa na uwezo nikaifanyia kazi kwa kuwekeza kadiri ya uwezo wangu. Vijana wa mjini tusijisahau na kuhisi kwamba sisi ni kila kitu, mwanzo na mwisho. Tumshukuru Mungu kwa kutujalia nchi tajiri yenye ardhi nzuri na rasilimali za kila aina. Tuamke na tufungue akili zetu, tuanze kutoka nje ya Dar es Salaam kutafuta fursa zilizopo mikoani. Tupeleke tulichojifunza hapa mjini kwa wenzetu na pia tuwe tayari kujifunza kutoka kwao. Tusisubiri wawekezaji wa nje waje kuwekeza hapa nchini, wengi wao watakuja kuvuna tu na mchango wao katika kuendeleza nchi utakuwa mdogo sana ukilinganisha na mchango wetu wenye uchungu na Tanzania yetu 🔚🙏🏼

1 comment:

Anonymous said...

It is all true alichokisema huyu kaka. Tuamke jamani fursa zipo nchini kwetu nyingi sana tena mno. Wageni wanaziona sana na kuzifatilia kwa nn sie wenye Nchi yenye kila neema tushindwe?