Genuine Nordic Vodka

Genuine Nordic Vodka

Tuesday, April 7, 2015

THIS IS VERY INTRESTING!!!




Takwimu za mamlaka ya mapato nchini (TRA) zinaonesha kuwa Mkoa wa Shinyanga ni wa 4 kuchangia pato la taifa ukitanguliwa na Dar, Mwanza na Mbeya. Lakini ni mkoa wa 11 kwa maendeleo.
Mkoa wa Arusha ni wa 7 ktk kuchangia pato la taifa, na mkoa wa Kilimanjaro ni wa 9. Lakini mkoa wa Arusha ni wa kwanza kwa maendeleo na Kilimanjaro ni wa pili.
UNAELEWA NINI?
Ni kwamba Shinyanga inachangia sana kwenye pato la taifa lakini haiendelei. Arusha na KLM hazichangii sana pato la taifa lakini zimeendelea.
Yani Shinyanga kuna hela lakini watu hawaitumii kwa maendeleo ya Shinyanga. Watu wanatafuta hela Shinyanga bt wanaenda kujenga sehemu nyingine.
Kilimanjaro na Arusha zinachangia kidogo kwny pato la taifa lakini zina maendeleo makubwa sana. Maana yake ni kwamba Kilimanjaro na Arusha hamna hela; lakini watu wake wanaenda kutafuta hela mikoa mingine then wanaenda kujenga kwao. Ndio maana Arusha ni ya kwanza kwa maendeleo na Kilimanjaro ni ya pili.
Itz paradox kuwa mkoa wenye maendeleo makubwa unachangia kidogo kwny GDP na hata Per Capita Income yake ni ndogo. Lakini mkoa unaochangia kiasi kikubwa kwny GDP & Per Capita Income ni kubwa mkoa huo ni maskini.
One of the reason ni unequal distribution of national cake, lakini other basic factor ni kuwa watu wa mikoa ya Kilimanjaro na Arusha ni watafutaji sana.
Takwimu hapo juu zinaonesha kuwa watu hawa wanaenda "kuchuma" kwenye mikoa yenye pato kubwa kama Shinyanga kisha wakipata wanaenda kujenga kwao.
Ni kawaida kumkuta mchagga anaishi chumba cha kupanga Singida akiuza supu ya mbuzi; lakini ana bonge la jumba kule kwao mgombani. Kwa lugha rahisi ni kuwa kumkuta mchagga akitafuta hela Lindi, Kigoma, Tarime, Geita ni kitu cha kawaida. Lakini kumkuta Mbena au Msukuma ana duka Moshi ni maajabu.
Nadhani watu wa mikoa mingine wanaweza kuiga spirit hii ya wachaga ya kwenda kutafuta hela popote inakopatikana na kuitumia kuendeleza kwao. Leo Kilimanjaro na Arusha ndio mikoa pekee isiyo na "vijiji".
Panapoitwa "vijijini" kuna umeme, barabara za lami, nyumba za kisasa, maji ya bomba etc. Kitu pekee kinachokuonesha hapa ni kijijini ni mashamba ya migomba na kahawa kila mahali.
Tungekua na Wanyiramba wanaotafuta hela Mtwara, Songea, Batiadi etc kisha wanazitumia hela hizo kwenda kujenga kwao Singida basi mikoa yote tungekua na maendeleo yanayoshabihiana.
Ila kwa mfumo wa sasa acheni Kilimanjaro na Arusha ziwakimbize.. Big up kina Masawe, Kimaro, Kaaya, Sarakikya, Laizer etc. Nendeni mkatafute hela huko Dar kwa kina Ficky Makame na huko Shinganga kwa kinaManawa Bukwimba halafu mkapige mijengo mikali kule Kirua, Machame, Meru, Old Moshi, etc. Hadi waelewe kwanini mlima mrefu kuliko yote Afrika uliwekwa kwenu badala ya Ludewa.!
Alamsiki,
Malisa GJ.!

1 comment:

Anonymous said...

Good read, going to shy to get a piece of that cake!