Genuine Nordic Vodka
Wednesday, April 8, 2015
READ!!!
GAIDI MTANZANIA SHAMBULIZI LA GARISSA NI MWENYEJI WA MWANGA
Taarifa zijazo end elea kutolewa na vyombo vya
usalama vya Kenya zimesema Rashid Charles Mberesero aliyekamatwa kuhusika na shambulizi la kigaidi lililofanywa na wapiganaji wa kikundi
cha Al-Shabab kwenye chuo kikuu cha Carissa
ambapo watu 148 wameripotiwa kuuawa,
anatokea Usangi katika wilaya ya Mwanga mkoa
wa Kilimanjaro.
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Kenya amesema kwamba Rashid alikamatwa akiwa amejificha juu
ya dari la moja ya majengo ya chuo cha Garissa ambapo baada ya uchunguzi ilidhihirika kuwa hakuwa mwanafunzi wala mkaazi katika chuo
hicho. Pia alipokamatwa alipatikana akiwa na
mabomu kadhaa ya milipuko.
Kufuatia taarifa hizi Mbunge wa Mwanga ambaye pia ni Waziri wa Maji, Profesa Jumanne
Maghembe alisema “Nimeshtushwa sana na
taarifa hizi. Ninaufahamu ukoo wa Mberesero ambao wanafamila wake wengi ni wakristo. Kwa wakati huu ni vyema tukaviachia vyombo vya
usalama kufanya uchunguzi wa kina kuhusu suala hili”.
Mtu mmoja: Huyo mbunge haijui familia hiyo vizuri, anatafutia
tu mahali pa kutokea. Usahihi ni huu hapa: Rashidi Charles ni mjukuu wa mzee Mberesero mmiliki
wa kampuni ya Ngorika bus, kwao ni Kisangara
Mwanga na siyo Usangi. kinachoshangaza siyo
dini bali utulivu aliokuwa nao huyo kijana, huwezi
kudhania ni kwanini amejiingiza kwenye vitendo hivyo kwavile kama ni swala la pesa kwao zimejaa, ama kweli umdhanie siye ndie.
Mchangiaji: Sasa, huyo Rashid Mberesero ni mtoto wa Charles Mberesero wa mke wa nje, na nasikia anasema walifunga chuo Dodoma wakaenda Kenya kwa ajili ya kuvamia chuo cha Garissa, huko Kenya walikutana na wenzao (wasomali) na ilikuwa tarehe tano wavamie uwanja wa taifa dsm kulikuwa na tamasha la pasaka.
Hawa Mohammed Adan Surow, Osman Abdi Dakane, Mohammed Abdi Abikar, Hassan Aden Hassan na Sahal Diriye Hussien,watuhumiwa watano wa shambulizi katika chuo kikuu cha Garissa ambapo watu mia moja na arobaini na nane walipoteza maisha,hapa wakiwa mahakamani,,source bbc!!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
3 comments:
it sounds more like speculations than factual information.
Taarifa hizo ni kweli na leo mahakama ya Kenya imesema Mtanzania huyo ataendelea kushikiliwa kwa mwezi mzima, kwa upelelezi zaidi. Ila kwenye hizo picha hayupo na wala huyo aliyevaa tshirt nyeupe sio yeye. Huyo ni mmoja wa attackers waliouawa siku ya tukio na ni mtoto wa chifu na civil servant maarufu huko Kenya. Wengi wamesambaza picha hiyo wakidhani ndio Mtanzania yupo na wala picha yake haijaonyeshwa.
AHSANTE MDAU KWA KUTUJUZA,,
Post a Comment