Genuine Nordic Vodka

Genuine Nordic Vodka

Friday, April 10, 2015

OH DEAR LAND OF TANZANIA!!!



Jana niliandika juu ya mgomo wa madereva uliopangwa kufanyika leo. Nikasema serikali ya CCM ikae nao na kuwasikiliza madai yao ili watafute suluhu ya pamoja. Lakini Jeshi la Polisi likaSHUPAA eti hakuna mgomo. Leo polisi wamejazana stand za mabasi na mitutu ya bunduki kulazimisha madereva wasigome.
U know what happened? Mbeya, Njimbe, Iringa, Sumbawanga, Tunduma, Mwanza madereva hawajatokea kbs stand. Polisi wameduwaa tu na bunduki zao.. Dar madereva wameenda stand wamewasha magari wakayaacha silent wakashuka wakapotea. Mipolisi ilivyo mijinga nasikia inawatafuta madereva popote walipo na luwalazimisha kuendesha magari.
Hebu imagine dereva wa Mwanza - Dar ambaye hadi sasa hajatoka, unamlazimisha aondoe gari kwa mtutu wa bunduki bila kumsikiliza madai yake, hivi akifika Sekenke akaamua kulitupa gari mtoni na kuua abiria wote nani wa kulaumiwa? Polisi hebu acheni utoto wa kutumika kama wanasesere. Mnashupaa kuwa gari lazima ziondoke leo, so what? Ishaurini serikali isikilize madai ya madereva sio kushupaa kuwa madereva lazima waendeshe magari. Kushupaa ni tabia imfaayo MPUMBAVU.! BY MALISA GODLISTEN,,

Hiii nchi inamatatizo sana...hatutaki kusikiliza shida za watanzania wa kawaida ...tunaona njia
ni kukamata viongozi ambao wanawakilisha tuu
watu nyuma yao. Tatizo la madereva lipo mda mrefu...ajira zao zimedharaulikaa...ila hatujui
services zao zina impact kubwa saana kwa jamii ya watanzania wa kawaida...sasa wanakaa tu viongozi washenzi wanapanga tu mambo ya
kipuuzi..dereva daladala hawezi kujisomesha kila ana renew leseni wakati ye nikibarua....tu sipende kuwatumia watanzania wenzetu kama toiletpaper..ukisha chamba basiiii hana tena maana...C.c David Jombi





MATOKEO YAKE NDIO HAYA MWISHO WA SIKU,,
PICHA ZOTE KWA HISANI YA EATV FB PAGE,,

UPDATE;;;MGOMO WA MADEREVA WAMALIZWA
Waziri wa Kazi na Ajira Mhe. Gaudencia Kabaka amefanikiwa kumaliza mgomo wa madereva baada ya kutangaza kufuta agizo lililokuwa likiwataka madereva wa mabasi na malori kwenda kusoma tena katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT)
Kuhusu suala la Madereva kusoma, Serikali na Madereva wamekubaliana kukutana mwezi huu tarehe 18 kuzungumza njia mbadala ya kutumika.
Miongoni mwa malalamiko ya madereva ilikuwa ni kukerwa na tochi za barabarani, hivyo jeshi la Polisi wamekubali kuziondoa.
Pia serikali imeagiza Madereva wote wapewe mikataba ya ajira za uhakika na waajiri wao na Trafiki wameagizwa kulifatilia hilo.

1 comment:

Anonymous said...

na matochi ya barabarani eti nayo yameondolewa....sijaelewa hili