Genuine Nordic Vodka
Friday, March 27, 2015
ADAM JUMA SAID!!!
Hizi vita za katika sanaa za kijinga sana, hazileti maendeleo bali chuki tu. Vita kati ya madirector sio jambo lakushangilia hata kidogo, kwani mtu ukiwa wa kwanza wa pili maana yake nini? Mnapoteza urafiki kwa ummaarufu wa siku mbili. Kitu hiki kilifanyika kwa pfunk na mj, then dunga na mapigo then lamar, wako wapi hawa watu ambao ndio mngongo wa mziki. Ukiwaangalia hawa maproducer wote ni wakali ila ujinga ndio umesabisha ubishani usiokua na maendeleo. Tujifunze kupenda na kuangalia style za wenzetu sio kwa lengo lakusema nani ni mkali au nani ni wakwanza, kwa nia hiyo tutakuza sanaa. Sijawahi hata siku moja kufikiria kwamba nimfunike mtu flani au niwe on top, bali nafanya kwa kadri ya uwezo wangu kuwa tafauti mengine nawaachia watazamaji. Sitaki kufananishwa na mtu yoyote yule kwa uzuri wala ubaya, kama hujaelewa nachokifanya nunua camera fanya wewe. Nawaonya nyie mnaogombana mkiwa mmesahau mlipotoka, UMOJA NI NGUVU UTENGANO NI UDHAIFU. Hakuna aliyebora kati yetu wote tunaudhaifu wetu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment