Genuine Nordic Vodka

Genuine Nordic Vodka

Monday, November 10, 2014

I GOT THIS ONE FROM EDWIN,,SPEAK YOUR MIND!!!


1.Uko ndani ya ndoa,mwaka wa kumi sasa na hamjapata mtoto,mkeo hospitali zote kamaliza na anaambiwa hana tatizo,kila akikwambia na wewe ukapimwe hutaki unajidai huna tatizo,ndo nini sasa hiyo? Kwa nini usipimwe mkajaribu IVF?
2.Ukienda Rose Garden we ndo Maprosoo kazi kuzungusha raundi huku ukijidai kusema...'uza nyumba utunze heshima bar'....asubuhi mwanao akikwambia 'baba shati la shule limechanika'..unakuwa mkaaaaaali,hovyooooo!
3.Umetoka zako kwenye mipombe,ni saa saba za usiku ,mama siku nzima mihangaiko kachoka we ukifika kitandani na ny....zako unamrukia tu bila hata maandalizi....ku ku...ku .....aaaaaaaagh....halafu huyo unakoroma,yaani mpaka mkeo anaona ka alikuwa anaota hivi,jamani hiyo sio baiskeli ya gym huyo ni binadamu ati.
4. Mnawaita beki tatu ma haus geli hao,juu ya nini unajipoza kwa mtumishi wa ndani? huoni unamdhalilisha mwenzio? Hivi ukibambwa utasema nini?
5.Ulipompenda ulimkuta ana kakazi kake,we na miwivu yako hutaki afanye kazi unamwachisha,hivi una uwezo wa kumpatia mahitaji yake yote yakiwemo matunzo ya wazazi na ndugu zake? Halafu kwa nini utake mwenzio kazi yake iwe kusafisha makochi na kuangalia plasma wakati wewe uko bize unachangamsha mwili na akili? Kufanya kazi au biashara is more than kuingiza kipato ,na ku interract na watu pia is healthy.
6.Mkeo akikusoea unaanza kumtangaza kwa watu... kwenye fb twitter whatsapp 'mkeo wangu sijui yukoje....mara hivi mara vile.....huoni unajiaibisha mwenyewe?
7.Na hizo nyumba ndogo hizo,ukienda huko kazi kumsimanga mkeo,matokeo yake siku mkeo akigombana na hawara yako anashangaa matusi anayovurumishiwa...we nae mwanamke wewe...si kikojozi wewe....du toba yarabi!
8.Ukiumwa kidogo tu full madeko yaani unajitia hata kidole huwezi kukisogeza,mwenzio serious tumbo linamsumbua,hata kusema ngoja nikae ndani nimuuguze mwenzangu ndo kwaaaanza unawahi kaunta Jackies,sana sana unampigia simu dada yako akamwangalie wifi,inahuu kwani yeye ndo kamwoa,akilalamika mkeo unamsimanga eti anadeka.
9.Nje utembee sasa ndo hata kuzaa uzae kabisa huko? maduka zinakouzwa condoms huyajui? au utasingizia ilikupasukia,na wa pili nayo ilipasuka? acheni hizo!
10.Huko kwenye mabaa na huo upuuzi unaoongelewa huko ....eh chapati shurti ikaangwe pande zote...sijui nini sijui nini...unarudi nyumbani na mipombe yako unataka ujaribu upuuzi wako kwa mkeo,peleka huko ujinga wako.
11.Umelala nje asubuhi unajitia kurudi nyumbani umefungwa pingu ili mke aone ulilala kituoni,mambo ya 1947 hayo,kinamama hawadanyiki na hizo siku hizi!
12.Mpira ..mpira...mpira....hamchoki? wikiendi nzima uko bar unaangalia mpira ,jumamosi man city vs man u,jumapili Arsenal vs chelz, weekdays kazi,hivi lini unakaa na kukagua kazi za watoto za shule? lini unakaa na mke na wanao na ku chat nao? mpira ndo utakaokuzika?
13. Ubinafsi wako huo,ukikaa sebuleni remote control haiko mbali na wewe unabadilisha tu chanel,si umuulize mkeo au wanao kama nao kuna kitu wanataka kuangalia? kuna mtu aliwahi kusema eti wanaume huona remote control kama ni extension ya mb....zao.
14.Sijui ndo umepiga wapi kabomu kako cha kwanza unamnunulia hawara yako ka vitz wakati mkeo anapanda daladala,kha!
15.Mke akilalamika mitabia yako mibovu unaanza..'kwani unataka nini..gari nimekupa..zaabu nakununulia...frigi imejaa chakula...kelele za nini? kwani kwao hakuacha chakula? yeye alikufuata wewe ati na sio plasma yako.
16. Unagonga wanawake wa nje kwenye kitanda anacholala mkeo na watoto hapohapo ni akili au matope? MJIPANGE NA MBADILIKEE.....
LikeLike ·  · 

4 comments:

Anonymous said...

hahaha nampendaje huyu kaka kaongea ukwel mtupu.

Anonymous said...

ukwelii mtupu.. ndoa za kibongo bongo mbona majangaaaa, mwanzoni nilikua napata presha sijaolewa mapema but now nimeolewa na foreigner nakula raha ya ndoa mnooo...half of the pipo i used to envy ndoa zao ziko chalii!!!

Anonymous said...

Huyu Kaka kasema ukweli kabisaa,Mdau wa 5:10,usiseme ndoa za kibongo bongo ni majanga sio zote wee mshukuru na umtangulize Mungu katika ndoa yako haijalishi umeolewa na foreigner au mbongo

Anonymous said...

Kwani kuolewa na foreigner kuna vigezo gani, kuwa ndoa zao ziko fresh na hazina migogoro...Acha ulimbukeni na ushamba. grow up