Genuine Nordic Vodka
Sunday, July 27, 2014
MADA YA LEO!!!!
NIMEBLOG KWA MDA MREFU SASA NA KAMA NI WATU WAPYA AU WA ZAMANI NADHANI MMEONA NINAVYORUSHA WANAWAKE WAKITANZANIA SANA TENA MNO,,
SASA LEO NILIKUWA NATAKA KUJUA KUTOKA KWENU NA HII MADA KUMBUKA NI SIO MASHINDANO BALI NI OPINION MAANA SISI WOTE NI WATANZANIA,,
SWALI LANGU NI KWAMBA MNAONA NANI WANAJUA KUVAA ZAIDI AU WANAFUATILIA TRENDS ZA FASHION SAHIHI JE NI WANAWAKE WANAOKAA TANZANIA AU NJE YA TANZANIA NA JE KWANINI,,
NATAKA UTOE CONSTRUCTIVE opinion YAANI USITUKANE MATUSI SITAKI NATAKA MUONGEE VIZURI KAMA MNAONA HAWA WANAVAA VIZURI NA USEME KIVIPI NA KAMA UNAONA HAWASTAHILI ANDIKA KWA UZURI KWANINI,,NIMEMALIZA.COM!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
12 comments:
Wabongo wa tz wanajua zaiidi yan hao wa nje siwaelewagi cjui ndo kujua kwingi
Wabongo wanavaa ila tatizo hawajui dressing codw. Yani hawajui nivae nini wapi. Kwahiyo wakati mwingine wanakuwa kituko tu. Ulaya muda mwingi watu wapo kwenye mabox. Lkn to be honest wanajua wavae nini wapi. Bongo mtu unakuta kavaa jumpsuit harusini. Au kirenge kwenye award(sikatai km imetangazwa ndio dressing code) na kuna vitenge matata sikuhizi ila kuna mwingine akitokea unataka kuingia uvunguni. Kwakweli bongo tunahitaji kuelimishwa swala la dressing code. Halafu watu wanavaa makorokoro mnoo. Yani naomba niishie hapa kwa sasa.
watanzania waliopo dar wengi sana wanajua kuvaa kuliko walioko nje ..... alafu wadada wengi tunaoishi nje tunafikiri kuvaa uchi its a fashion but i thinks to be classic is fashion and fashonist wengi wakubwa wa dar wanajitahidi kwenye hilo swala na wanasaidia wengine kuwa hivyo
Mimi kama mfwatiliaji mzuri wa blog hii,naona kwanza wanawake wengi unaowarusha humu wako bongo. Hiyo peke wake inawapandisha zaidi. When it comes to wanaojua kuvaa obviously tulio nje tunajua zaidi sio kwasababu tuko nje but tuna access kubwa zaidi ya nguo nzuri(nofakezone) na kwa affordable prices!!!!!!! Kwa bongo nawakubali ni
JAKI MAMA WAWILI NTUYABALIWE
KIKI
JACKY WOLPER
FARAJA KOTTA
NANCY SUMARI.
Wanawake unaowaweka huku nuru ni macelebrities not everyday pipo. Ulaya hatuna muda wa kuvaa na kupendeza kila siku, schedule utamwachia nani???? Bongo raha everyday all day,wengi wako kupendeza ndo MTAJI WAO sasa wataacha kuvunja makabati kweli????
Main point ni kwamba, wa tz walio bongo wengi hawana kazi za kufanya zaidi tu kujipodoa kutwa nzima, wa tz wa nje box kali huo mda wa kujipodoa na kujitundika mitandaoni hawana.. Na pia ikumbukwe kuwa hao wanaojua kuvaa bongo wengi ni wadada wa mujini.. Wenzangu na mie wakutoka ileje hakuna kitu. Na ukumbuke walio nje wametoka mikoa yote tz, pengine wamekuja soma n.k. Huo mda wa kujisexisha hawana na pengine hawajui kwani sio wadada wa mujini. Wadada wa mujini walio nje mbona wananyuka, eg. Dada Sporah, Mk, Teddy K, Norah, Bella na dada mmoja yupo scotland. Nuru the light, N.k na pia bongo dada ya mujin wako wengi kuliko nje, so ni rahisi kuwa noticed.
Kwa kweli bora umesema nuru,kwa miaka ya nyuma ningekubali wanawake walioko nje walikuwa wanajua kuvaa but of recently my dia na sisi tumeamka tunavaa mno hapa kwetu sana tena sio kidogo,example unakuta msanii wa bongo kaenda majuu kwa show lakini ukiangalia zile mapicha gooosshh!! Yaan wamevaa maronya nguo haiendi na body shape of which kule ndo kila kitu kina originate mabody shapers ma spanx yapo bwerere lakin kava nguo haijamkaa fresh lakin sisi bongo bana nowadays tunaorder toka huko tunavalia munooo!!!
AHSANTENI KWA KUCHANGIA MADA NLIKUWA NATAKA KUMJIBU TU MMOJA WENU KUWA UKISEMA NAWARUSHA MACELB TUU UNAKOSEA SIDHANI KAMA KUNA BLOGGER ANAYERUSHA WANAWAKE WAKITANZANIA KAMA MIMI KWENYE BLOG YAKE NA TENA WALA SIO MACELEB BUT STILL NAWAPA NAFASI HUMU,,MIMI NKIONA MTU KAPENDEZA I SHARE IT WITH PEOPLE NAPENDA SANA WANAWAKE MTU APATE IDEA YA KUJUA KUPANGILIA MAVAZI NDIO MAANA NARUSHA WANAWAKE TOFAUTI FOR EXAMPLE DIFFERENT BODYTYPES,SIZES NA MENGINEVYO,,NA MDAU ULOSEMA NAWARUSHA SANA WALIOPO BONGO NTALIFANYIA KAZI PIA LA KUWARUSHA WA ULAYA.COM PIA,,
Na pia hali ya hewa, nje mara nyingi ni baridi, watu kutwa makoti.. tofauti na bongo 24/7 summer mtaacha kuonekana mmependeza? Ila mlio bongo jamani hasa hawa bongo movie na mashughuli blog, hizo make up!!! Uwiiiiiiiii yaani kama vinyago.
Kuna this gal anaitwa Neema Wanyancha Na Yule Swalha Wanajitahidi Sana Pia, Nimezungumzia Kwa Upande Wa Bongo Hapo.
Tukirudi Kwenye Point Mie Naona Wanakaribiana Ila Wabongo Sometimes Wachache Wao Wanakosea Dress Code, Hawajui Vazi Hili La Wapi Na Hili Wavae Wakiwa Wapi.
We uliyetaja wa Ileje umeniboa. Swali ni je wapi wanaojua kuvaa wa ndani au wanje ya Tanzania?
Hukuulizwa wa wilaya au kabila gani.
Samahani najuwa Wanawake mkiongea mtakuwa Kama mnapendeleana au kujipendelea kujitetea mngetuwacha sie Wanaume pia tuongelee hili, Wanawake ambao Mie kwa maoni yangu na nipo nje ya nchi nafikiri kwa Wakitanzania ni Waliopo nchini Tanzania ndio nimeona wanavaa vizuri na si sababu ni Celebrity ila mpaka sasa Napenda Faraja Kota na Nacy wanavyovaa Classic wanavaa na Nargis pia napenda anavyovaa wanajiheshimu wa nje wengi wanavaa nguo fupi na fupi hizo si kwamba zinaendana na mtu unaweza Kuwa Mguu Mnene na Mguu mwembamba zikakupendeza ila wengi tofauti na inavyotakiwa kuvaliwa, nje wengi nimeona mavazi ya Club na Harusini basi ila kwa wanaosema wengi wapo na muda wa kazi za Box siwalaumu mnavyo point ila swali la jibu ni Watanzania wanajuwa kuvaa Mie napenda movie za Black and White na za 1950 kila nikitizama Nancy na Faraja wamekamilika Kuwa kwenye Movie za 1950. MZ
Post a Comment