Kuongezeka Kwa Matumizi Mabaya ya Mitandao ya Kijamii!
kwenye moja ya post zangu ameniuliza nini kauli yangu kuhusu matumizi mabaya ya mitandao , picha chafu na za kutisha na kuingiliwa faragha!
Nimemjibu hivi:
Matumizi mabaya! Faragha kuingiliwa! Unakumbuka kampeni ya FUTA delete Kabisa? Ninachoweza kusema ni kutokuelewa na kutofahamu na wakati mwingine (samahani situkani) ushamba na ujinga wa kutozingatia masharti ya matumizi ya mitandao. Soma humu masharti ya matumizi ya Facebook, mitandao yote ya kijamii ina masharti ila watumiaji wachache, narudia, watumiaji wachache wanajiunga bila kusoma hayo masharti wanatiki tu box "I agree" bila kuelewa.
Na sisi tungekuwa tumesoma tungeona sehemu inaelekeza utoe taarifa kwa moderator uonapo jambo linaloenda kinyume, picha chafu, habari zisizo na ukweli nk. Richard Mabala umewahi kufanya hivyo.?
Internet Regulation ni challenge duniani kote. Inahusika na behaviour (tabia) za watu. Unapokuwa wewe mwenyewe unauelewa mdogo (wengi ya watumiaji) wame "lip frog" kuingia matumizi ya mitandao. Unayoyaona Facebook au mtandao wowote wa kijamii ni hali halisi ya Jamii yetu. Hii ni platform tu ya kuibua hali halisi ya uhalisia wa yaliyomo kati yetu.
Ushauri: Tuanze nyumbani, fundisho kwa watoto na familia, wawajibike kutumia vizuri mitandao, tukemeane tunapoona mtu anaweka kitu kibaya. Tuzingatie masharti na kanuni za matumizi hayo. Mungy au Mabala au hata Jeshi la polisi linaloshughuliia makosa ya jinai na uhalifu hawawezi wenyewe. Tcra inatoa leseni kwa watoa huduma za Internet sio watumiaji.
Tusaidiane, let's shame them, watumiaji wabaya, tufute na ku delete upuuzi, picha chafu na tuache (samahani tena) ushamba wa matumizi ya mitandao. Wenzetu wanaotumia kujifunza, kubadilisha mawazo na kujenga mahusiano, sio kubomoa.
Kila mtumiaji anawajibika, wewe na mimi. Tufanye "Polisi Jamii Shirikishi) kulinda matumizi ya mitandao. Tu report picha chafu, picha za kutisha, zinazodhalilisha utu na ubinadamu. Kataa kuwa "tagged" kwenye post usiyoikubali. Unfollow Na block marafiki wenye kutumia mitandao vibaya.
Najua haitoshi, lakini tuanze hapo! Nafahamu nimekera baadhi yetu! Chukua hatua, pinga matumizi mabaya ya mitandao.
Toa taarifa kwenye page ya funs wa FUTA Delete Kabisa ya Facebook kwa kuwakanya wanaotumia mitandao vibaya. Kuwa Balozi wa matumizi mazuri ya mitandao.
No comments:
Post a Comment