Genuine Nordic Vodka

Genuine Nordic Vodka

Thursday, July 3, 2014

FACEBOOK STATUS BY ZUBEDA!!!




Ila baadhi ya watanzania tunafurahisha sana , kijana wa watu mdogo Daniel Lema( Rest In Peace), mmemchoma kwa kudhaniwa mwizi ila jamaa wa ESCROW hata kuwapigia kelele za 'mwiziiiii' pamoja na kuambiwa wameiba? Tutabaki siye watu wa matabaka ya chini kuuana kwa kuku, simu ya tochi.... ila jamaa wa EPA, sijui rada (hawa wezi walijulikana na wakasamehewa eti warudishe chenji, nasikia hela walienda kununulia vitabu vya shule**vitabu vyenyewe vinasema 1 x 5 = 15) mob justice inafanya kazi kwetu siye masikini, tutamalizana wkt wengine wananeemeka na kodi zetu.... Eniwei, nilitaka kusema kuwa woga wetu ndo umasikini wetu... Tutamalizana wanyonge,wakati wenye akili nchi hii wanajumlisha 1 + 1 = 11 katika mikataba, tenda, manunuzi, matumizi na naniliiino yaani kwa makusudi kuongeza 000 kwenye hela za walipa kodi si wizi... gari ya milioni 40 inafanyiwa sevisi ya milioni 95, halafu mnaua wengine kwa kudhaniwa wezi.. Ps:Meno yangu nimeshayapiga ribiti na kucha nimezikata tayari plas nywele nimekata, macho mabovu ndo mana navaa miwani.: dont wore mai frens!

No comments: