Mwandishi: Millen Magese Foundation inatoa huduma gani kwa upande wa afya?
Happiness: Katika suala la afya tumejikita zaidi katika hali ya kiafya ya maumivu ya mwanamke katika hedhi ambayo inajulikana kitaalam kama ‘Endometriosis’.
Ugonjwa huu umeshanikumba na napenda niweke wazi kwa maana ni vyema mtu akianza mapema hawezi kuwa na matatizo yaliyonikumba.
Nimeshafanyiwa upasuaji mara 12 na mirija yangu yote imeziba, upande wangu mmoja wa ovary haufanyi kazi. Ile ndoto yote ya mimi kama mwanamke kupata mtoto kwa njia ya kawaida imetoweka.
Nisingependa kuona wanawake wengine wanakwenda njia niliyopitia na ndiyo mana nipo hapa Tanzania ili kuweza kuliongelea zaidi na kuiomba hata serikali, vyombo vya habari watu wote kujitolea kuweza kumsaidia mwanamke huyu ambaye anaweza kuwa kama mimi.
Ukimsaidia mwanamke utakuwa umesaidia dunia nzima. Mwanamke ni nguzo katika nyumba yoyote ni suala ambalo linapaswa kuongelewa na wababa, wakaka na viongozi kila sehemu.
Nimepanga kutoa semina mbalimbali kwa wanawake, ikiwezekana kufungua hospitali maalum ya wanawake itakayotibu ugonjwa huu.
Mwandishi: Tangu umeanza kuutibu ugonjwa huu wa Endometriosis, umetumia kiasi gani?
Happiness: Nilianzia Afrika Kusini ambako nilifanya operesheni 10, mbili nimefanyiwa Marekani. Gharama ya Afrika Kusini ilikuwa ni randi 35,000 (sh milioni 5,500,000) kwa Marekani ilikuwa ni dola 6,000 (sh. milioni 9,958,000).
Halafu kuna vitu ambavyo unatakiwa uvitumie kwani kuna kuwekewa mayai na unachomwa sindano 63 kwenye tumbo, kila siku unachomwa sindano tatu kwa siku 22 na kila siku unaamshwa kwa ajili ya kufanyiwa Ultrasound, nadhani unaona maumivu ni kiasi gani unayapata. Kwa bahati mbaya mwili wangu uliweza kuzalisha mayai matatu kwa sababu ovary yangu moja haifanyi kazi wakati wengine wanazalisha kuanzia saba mpaka 15.
Magese akielezea alivyoteseka na Endometriosis.
Endometriosis kwangu imekuwa sugu ndiyo maana msishangae siku nikienda Italy, Marekani au sehemu yoyote kuasili mtoto, hii ni kwa sababu Mwenyezi Mungu ndivyo alivyonipangia.
Mwandishi: Changamoto zipi unakumbana nazo katika fani ya uanamitindo?
Happiness: Changamoto yangu kubwa ilikuwa ni afya yangu.
Nilikuwa sijui lini nitakuwa okey, lini nitafanyiwa upasuaji na lini nitarudi kwenye kazi yangu maana ukiondoka leo zinakuja sura mpya zaidi ya 1000 unashindwa kujua kama utarudi na kuwa top. Nashukuru nilipata viongozi wazuri wa kunisimamia na kuniongoza mpaka nimejulikana kama Happiness Magese na kuwa mwanamitindo maarufu.
Nawaomba waajiri wote muwaangalie watu wa namna hii na mkishamfahamu ana ugonjwa wa Endometriosis mpeni ushirikiano sana,,
KUNA MDAU ALITUMA HII COMMENT JANA ILA INAHUSIKA SANA NA HII MADA HAPA
mungu asidihie mara dufu dufu mileni anamroho safi dada huyu namzimia sana xaxa wale mafala waliokua wakimsema humu eti mileni huzai unazeeka cjui miaka inaenda nk sura mtaziweka wapi?msiwe wepesi wakuwasema wenzenu kwa ubaya na kuwaombea mabaya hujui mtu anapitia changa moto gani mpk akawa hana mtoto.dada milen anaugonjwa hawezi kupata mtoto wengine hawana kizazi kuna wengine wamefanyia ma surgery mpk wamepata anagalau katoto kamoja wengine wameamua kuadopti jamani tubadilike usiombe mwenzako utasa nawakati bado uhai mungu analipiza tena kwa kasi zaidi na vile tunavyo fikiri hata kwa wale wenye watoto wengi hujui maisha ya mbele yakoje kuna kifo kuna maradhi nk tusiombeane mabaya kwani yanadurudia wenyewe inasikitisha sana jinsi gani watu hawana furaha ktk maisha yao wanatafuta faraja kwenye mablogu amtukane mtu amalize stress zake tubadilike.com
Source GPL