Genuine Nordic Vodka

Genuine Nordic Vodka

Thursday, May 22, 2014

FROM SAMSON SIBORA,JE DO YOU AGREE OR DISAGREE!!!!



Mimi sio mtazamaji mzuri wa Clouds TV kwa kuwa vipindi vyake vingi havina mvuto wala mafundisho ya maana. Jana, kwa bahati mbaya, nilitazama kipindi cha ‘BIBI BOMBA’ kinachorushwa na TV hiyo. Nimehuzunishwa sana kuona jinsi bibi na mama zetu wanavyodhalilishwa hadharani. Bibi zetu huulizwa maswali ya kidhalilishaji.
Bibi mmoja aliulizwa kama aliwahi kula mboga inayoitwa ‘Biology’, akajibu ‘ndiyo’. Hili ni swali linalohusu ufahamu na kwa wabibi wale ambao hawakwenda shule, hawajui biology ni nini. Si hivyo tu, hata wale walioishia la saba hawajui biology ni kitu gani. Kuwauliza mabibi swali kama hili ni kuwadhalilisha kitaaluma kwa kuwa tu hawakwenda shule.
Bibi mwingine aliombwa amtongoze kijana yule anayewauliza maswali hadi amkubali. Bibi akatekeleza agizo hilo laivu mbele ya skrini ya TV! Huu ni udhalilishaji wa hali ya juu.
Kama kweli kinachofanyika katika kipindi kile ni kuwajali bibi wale kwa maana ya kuwapatia pesa wakishinda hebu wanaoendesha kipindi kile siku moja wawalete bibi zao na wawahoji maswali yale ya kishenzi tuone kama itakuwa sawa kwao, kwanini pesa iwe kigezo cha kudhalilisha watu wazima? Tena wanadhalilishwa na vijana wadogo wasio na chembe ya maadili? Hivi kweli kumwambia bibi mtu mzima amtongoze kijana mdogo halafu mbele ya skrini kila watu wa rika tofauti wanatazama wakiwemo watoto hapo tunafundisha maadili gani kwa jamii?
Wizara ya jinsia inapaswa kukataza udhalilishaji huu wa kijinsia.
 Nasi wananchi tuache kushabikia upumbavu huu–tukatae kuwapigia kura bibi wanaoshiriki. KAMA WEWE UNAMJALI BIBI YAKO NA WABIBI WA TAIFA HILI TAFADHALI TUKATAE UNYANYASAJI HUU.

here are some comments,,

Wajifunze Kwa maisha plus na mama shujaa.
Mamlaka zinazo simamia mambo ya habari zimelala
Mbaya zaidi na watoto wanatazama tunatengeneza 'atomic bom
kama wanapenda kuwasaidia bibi zetu wafuate maadili yanayofaa kuigwa na jamii.na si kuwadhalilisha kwa ajili ya pesa

5 comments:

Anonymous said...

Money makes monkey dance.....that's what they say!

Anonymous said...

wallah hii ni kweli tupu.nimesoma hadi machozi yananitoka.iam really touched.

Anonymous said...

Amina umesema kweli kabisa, niliangalia hicho kipindi mwaka jana dakika tano tu niliudhika sana hizo mamlaka ziko wapi. Nasikitika wanafungia vipindi vya maana kama 'jicho la ng'ombe' ila huu udhalilishaji wa wazazi wetu wanaangalia tu, shame!

Anonymous said...

ni ukweli mtupu,clouds wamezidi jamani yani vitu vyao havina maadili mpaka basi ni ujinga na ujinga na ushenzi huyo ruge sijui anatengeneza hela halafu anaaribu watu wengine..!!!mie siwapendi clouds ever since back in the days when their were nothing

Anonymous said...

Alafu ndio mnasema watu Kama kina ruge Wana degree ndio wanaakili? Jamii imefika kuvunjiana heshima bila kujijua kwa pesa tu.