TAFUTA UFANISI WA MAISHA, SIYO UFANISI WA KULIPA KISASI
Kuna wakati huwa najiuliza, ni kwanini watu wanatumia muda mwingi kupanga mikakati ya kumdharau mtu fulani ilimradi tu ajue kuwa amedharauliwa.
Inaweza mtu huyo amekukera, amekuudhi, amekuchukiza na kukufanya upandwe na hasira na kadhalika.
Binafsi nimewahi kudharauliwa, kupuuzwa, kubezwa, kuonekana kituko na watu wa kika jinsia. Wengine wanafika mahali hawatimizi kile mlichokubaliana na mwishowe unaonekana kama mwendawazimu, lakini ukijijua kuwa uko safi.
Binadamu tunaweza kutumia nguvu nyingi kutaka kulipa kisasi kwa mtu aliyekudharau, kukupuuza na kadhalika, kwa lengo la kuridhisha nafsi tu basi.
Ukishalipiza kisasi cha kudharauliwa au kupuuzwa, basi unaona umefika na unajiona gangwe kweli kweli.
Ni kweli wapo wanaotudharau, wakakuona chizi na kukuonesha kila aina ya kejeli ambayo inachukiza moyoni.

Lakini jambo muhimu ni kuipumzisha akili yako, usipoteze muda wako bure kuhangaika kulipiza kisasa cha wanaokudharau au kukupuza.
Tumia nguvu nyingi kuijenga nafsi yako na muhimu fanya kazi yako kwa ufanisi kuliko kutafuta ufanisi wa kulipiza kisasi kwa wanaokudharua.
Kwanini mtu akipuuza maombi yako, akakukejeli, akakubeza, inakupunguzia nini.

Na wanaonibeza na kukejeli sipotezi muda, wala sihangaiki eti fulani amenidharau basi nitafute ufanisi kulipa kisasi.
Nina kazi nyingi za kufanya kuliko kujihangaisha eti fulani kanidharau au kapuuza makubaliano basi nilipize. Tabu ya nini? Shauri yako!
Wazo la kiandunje hili utaumia bure ukilibishia.
© Andunje wa Fikra,& FACULTAS, 2014.

No comments:
Post a Comment