USHAWAHI KUTIWA LOCK UP IN BONGO AU KUJUA MTU AMBAYE ALIWAHI PATA HII EXPERIENCE..,KWAKWELI MAPOLISI IN BONGO NI WATU WA AJABU SANA MAANA KAZI YAO NI KULINDA RAIYA LAKINI WAMEWEKA RUSHWA MBLE MNO KULIKO KITU CHENGINE CHOCHOTE.,
NNA MASWALI MACHACHE AMBAYO NTAYAULIZA NA NAOMBA MNISAIDIE KUJIBU MAANA UKISHAZOWEYA MAZINGIRA FLANI SISI BINADAMU HUWA TUNASAHAU WENGINE WANAIISHI VIPI.
1.HAKI YA BINADAMU,HIVI HIKI KITU KINAJULIKANA KWELI TANZANIA MAANA MTU UKITETEA HAKI YAKO UNAAMBIWA MBISHI,MJEURI NA MENGINE KADHALIKA!
2.JE WALE WANAOISHI NCHI HII BILA KUJUA WATU WANAWEZA KUJISAIDIA VIPI WAKIPATA SHIDA KISHERIA KAMA HAWANA HIZO CONNECTION WAKATI SYSTEM HAIKO KWA AJILI YA MWANANCHI!
3.NA WAGENI WANAOKUJA ITEMBELEA NCHI YETU WANASAIDIWA KIVIPI WAKIPATA MATATIZO!
MIMI NAPENDA SANA NCHI YANGU LAKINI KUNA MAZINGIRA NA VITU AMBAVYO NAVIONA NA KUNISIKITISHA SANA KIASI KWAMBA NIMEONA NIWAULIZENI WADAU MAANA NIMEKOSA MAJIBU NA KUBAKI NA HUZUNI!
6 comments:
Jamani mi nasema hivi, wacha hizi kazi za mabox ziniuwe kwenye hizi nchi za watu lakini HUMAN RIGHT ninayoinjoy you can never put a price tag on it. Yaani system zetu nyumbani Tanzania na pia na nchi nyingi tu hazieleweki, system inaweza badilishwa mara tu kama wewe ni mvuja jasho, lakini kwa wengine system inanyooka. Na pia hata kwa upande wa wanawake ndio usiseme tena lakini huku bwana uwe mtu toka wapi sheria ni sheria na inafwatwa na cha zaidi HAKI ZA BINADAMU zinafuatwa haijalishi kama wewe ni nani.
Pole Nuru, naamini tuko wengi wengi tunaosikitishwa na hili lakini ukweli ndio huo 'Pesa ndio inaongea'!! naona viongozi wachache wanajitahidi kupiga vita rushwa inabidi tuwaunge mkono siku moja tutafika..Mungu ibariki Tanzania
yani ndo hivyo Nuru, Sheria watu wanaijua ila hawaifati kwamakusudi ili kurahisisha maisha yao. Asie kuwa nacho ndo huwa anaumia daima, na kwa wale wageni ndo kabisaaaaaaaaa maana watanzania wanahisi kuwa mtu anaetoka nje ndo huwa anapesa so huwa wanafanya kama kucreate mambo ili wapate chochote kutoka kwake, kwa mfano ukihisiwa kuwa wewe ni mgeni utapandishiwa hata bei ya bidhaa , mfano kama chungwa linauzwa shilingi 100 , mgeni anaweza uziwa shilingi 200. Thats what am trying to mean.
Much luv.
pole sana mamaa,ni kwamba haki za binadam kule nyumbani ni kitu cha kusahau HAMNA,pili rushwa kwa polisi ni kama vile kunywa maji kwao,yaani ni haki yao na wala hawabishi wanaipenda na wanaitaka na ni lazima uwape,hivyo wakikukamata hata kwa kosa lolote ama kukuonea rushwa wataomba ama hata watakunyanganya wakiona mbishi kuwapa na hela unazo na mwishoni unaweza kuambulia kipigo.tatu mama unapokuwa unaenda likizo huko jaribu kusahau kidogo mambo ya sweden maana nchi yetu kwakweli imeoza katika nyanja zote,hivyo inabidi ujiandae na uandae vilevile fungu la zawadi(hongo) kwa ajili ya polisi na matrafiki km huwa unadrive.hapo utaenjoy life vinginevyo maisha yatakuwia magumu sana kule nyumbani.at last kwetu ni kwetu licha ya yote hayo utaendelea kwenda tu hata iweje,pole sana kwa maswahibu kama ulikutana na hao bin-adamu wanaoitwa polisi bongo.
Nuru askari wa TZ ni kama miungu flani hivi.Ni afadhali kidogo kwa mtu anayejua haki zake anaweza kuburuzana nao ila kwa wasiojua kabisa hali ni mbaya sana kwao.Wakati wote lugha zao ni za kitisho na hii ni ktk kuhakikisha kuwa wanajaza mifuko yao.Ukikomaa nao kuwa hutoi pesa wakupeleke kituoni wakifika na wewe kituoni wanabadilisha maelezo.System nzima ya TZ inahitaji mabadiliko.
dada tz imeoza kupita maelezo rushwa imeota mizizi kwa mapolisi ndio kabisaa rushwa kwao ni kama samaki na maji yaani rushwa wameizoea hawaoni hata kama nikukiuka sheria wao wanaona ni sehemu ya maisha yao tanzania kila idara imenuka bora ujikalie zako huko huko maana tz kichefuchefu tupu utafikiri hakuna viongozi wacha nikitaka kuandika uozo wa tz maelezo itatosha kitabu inatakiwa kila mtu asali kwa ajili ya tz maana ni balaa tupu
Post a Comment