Genuine Nordic Vodka

Genuine Nordic Vodka

Wednesday, June 8, 2016

EDUCATIONAL:IGBO LANDING!!!


Kwenye video ya Beyonce kuna hii scene amesimama mstarini na hao wengine na chini mnaona picha ya watumwa ambao waliletwa marekani wakati wako njiani waligoma kwenye meli na kuiteka huku wakiimba nyimbo za kabila lao Igbo na kuifikisha kisiwani
Walipofika walisema ni bora wafe kuliko kuwa watumwa na kujipanga mstari mmoja huku wakiimba na kuelekea majini na mwisho wake kufa huku wamezama.
Hiki ni kitendo cha ushujaa kikionyesha kuwa bora tufe kuliko Utumwa na ilikuwa mwaka 1803 kisiwani St.Simon in Georgia Marekani.

 WEUSI TUMEPITIA MENGI SANA KIHISTORIA ILA BADO HAWAJITAMBUI AS PEOPLE OR AS A RACE,BADO TUNA SAFARI NDEFU MNO NA SIJUI KAMA ITAKUJA KUWA A REALITY BUT BADO WEUSI NI WATUMWA KWENYE DUNIA HII YA LEO
SIMPLE FACT KWAMBA AFRIKA INALISHA DUNIA NZIMA BALI NDIO BARA LENYEWE NJAA INAKUINGIA AKILINI KWELI?
AFRICA INA MADINI NA MENGINE MENGI ILA  NDIO BARA MASKINI,REALLY?
BADO TUNAPIGANA NA UTUMWA NA MAUWAJI KIKABILA NA KIDINI SISI WENYEWE KWA WENYEWE JE INAKUINGIA AKILINI KWELI,,
AHH MY AFRICA INDEED TUNASAFARI NDEFU NA ALOTULAANI SIJUI NI NANI!!

8 comments:

Anonymous said...

Kiukweli umeongea ukweli kabisa Nuru wazungu bado wametukalia it means bado wanatutawala na hatujielewi, kiukweli Afrika ni bara lenye utajiri wa kila aina lakini bado maskini wenzetu wanakuja kuchota na kupeleka makwao sie tunateseka kwa kweli bado tuna safari ndefu na haita kwisha hii ndo majaliwa yetu ya kuwa watumwa ooh mungu tusimamie na kila baya tupate heshima zetu.

Anonymous said...

wow, this is powerful.... So glad now Beyonce has chosen to be more connected to her roots than pleasing the masses!

NURU THE LIGHT said...

Me too am glad shes making music with consious that teaches us about the history but also current event like the Police killing black systematically

Akija mmoja kutubeba wanakuja 100 weusi wenzake kumrudisha nyuma kama si laana ni nini?

Anonymous said...

You spoke the truth Nuru the Light

Anonymous said...

Education, Education, Education PLUS Hard Work

Anonymous said...

Yaani Nuru umeongea ukweli sijui bara la Afrika lina matatizo gani? Watu wake bado hawajielewi kabisa mpka karne hii, si ajabu kuitwa bara jeusi na watu wake weusi mpka miyoyo yao. Afrika ni bara tajiri sana kupita maabara yote kwa utajiri wa asili, Afrika ni bara kubwa la pili kwa ukubwa na limekaa vizuri, tena nchi zote zenye utajili wa asili zipo zimelala Afrika na Congo ndio nambari mmja inayongoza duniani kwa utajili wa asili, maajabu yake watu wake ndio masikini duniani, nchi masikini zimejaa Afrika, njaa Afrika ,magonjwa Afrika,kukosa huduma muhimu miundombinu Afrika, yaani ujinga ujinga wote umejaa Afrika, kutopendana, kujaliana uadui baina sisi kwa sisi Afrika na hivyo ndivyo vinavyosababisha tuwe nyuma na tuendelee na utumwa na wenzetu wanazidi kufaidika na kunemeka, tukija hamka tumeishiwa hamna kitu. Tunaendelea kuwa watumwa kabisaaa, manaake bara halijielewi hili

Anonymous said...

Hmmm Nuru umenichekesha kweli mpendwa hapo ulipoandika. Akuna mmoja kutubeba wanakuja 100 weusi wenzake kumrudisha nyuma kama si laana Nini? Hmmmm kweli sisi watu weusi tunamatatizo mpakaa, hata ukiangalia enzi hizo za utumwa ni hao hao weusi ndio kutwa walikuwa kuwavizia wenzao na kuwapeleka kuwauza, na kutwa vita vya wenyewe kwa wenyewe ukabila. Kabila likishindwa vita ni kupelekana utumwa mtindo mmoja, na miaka hiyo dini zilikuwa sio sana walikuwa tu na imani zao za asili kama sio mizimu sijui mahoka ni tabu bara hili, sasa sijui ingekuwaje kipindi hicho na dini hizi tulizoletewa kwetu ni mpya naona tungejiangali kama hayawani wa mwituni hapo ingekuwa peleka peleka tu hii mbona ni hayawani wa mwituni.

NURU THE LIGHT said...

Ndiomaana huwa naitumia sana slogan ya adui wa mwafrika ni mwafrika na mkombozi wa Africa ni Muafrika!!