Wednesday, May 13, 2015
I HAD A HUNCH!!!
Jumapili iliyopita Staa wa Bongo Movie,Kajala Masanja alipata mkasa wa kupigwa chupa na mtu asiyejulikana katuka klabu ya usiku ya Maisha iliyopo Masaki jijini Dar es Salaam katika shoo maalum ya kumchangia mke wa msanii Mabeste Venus, Lisa Karl Fickenscher iliyowakutanishamastaa wengi wa ‘category’ mbalimbali.
Habari zinasema kuwa wakati shoo hiyo inakaribia kumalizika majira ya saa alfajiri wakati msanii huyo akiwa na ‘kampani’ yake walitawanyika lakini wakati wakiwa nje ghafla jamaa mmoja ambaye hakufahamika ‘aliwa-join’ na kuwachangamkia kusiko kwa kawaida huku wao wakionekana kutompa ushirikiano aliouhitaji.
Hata hivyo, jamaa huyo ‘alifika mbele’ zaidi kwa kumshika makalio Kajala ambaye alimnasa kibao. Katika kujibu mapigo, jamaa huyo alimpiga na chupa ya bia kichwani na kusababisha jeraha usoni.
Baada ya tukio hilo Kajala alipelekwa hospitali na kupatiwa matibabu.
source;stephen ipyana blog
watu wamerogwa? unamshikaje mtu makalio bila ridhaa mbwa huyo
ReplyDeleteHuyo ni mpumbavu anampigajee mwanamke Chupa atafutwe apigwe kiberiti cha moto mkunduni
ReplyDelete