Genuine Nordic Vodka

Genuine Nordic Vodka

Wednesday, November 25, 2015

SOMETHING WORTH THINKING ABOUT FROM MWAMINI,KATIBA!!!



Kipimo cha uzalendo na uchapakazi Wa JPM sio kwenda muhimbili Bali ni kuheshimu maoni ya WanaNchi. Tunataka Katiba Mpya wenye maoni ya WanaNchi Aka Rasimu ya Warioba. Huo ndo Unga tuutakao sio uji Wa kuzuru muhimbili.
Mzungu anasema don't give me a fish teach me how to fish.
Kilio cha Taifa hili ni Haki na Usawa.
Tunaitaka hiyo haki iwekwe bayana Kikatiba.
Hatutaki danganya toto Leo Magufuli yuko ikulu kesho hayupo baada ya miaka 5 na isiyozidi kumi Itakuaje!?
Nini hatma ya Taifa hili je tusipo mpata rais Wa Utashi kama yeye itakuaje!?
Kuwa na maono ya Mbali na kujiuliza legacy yake. Italindwa vipi bila sheria mama!?
Asifanye makosa aliyoyafanya Mwl. JKN mwasisi Wa Taifa ( TANU & CCM) ya kutokufanya Azimio la Arusha na maadili ya viongozi Wa Umma kuwa kikatiba.
Matokeo take yalifutwa kirahisi sana kwa kukutana Zanzibar na kutoa Tamko LA kufuta maadili na miiko ya Utumishi Wa Umma. Hapo ndipo chama na serikali ya Mapinduzi zilipo poteza Dira.
Kama ingekuwa kikatiba isingewezwa futwa kinyamele na Halmashauri kuu ya Chama (NEC) iliketi mjini zanzibar kuirekebisha miiko ya Uongozi na kuazimia kuifanyia marekebisho yaliyojulikana kama Tamko la Zanzibar.
Kamati ya Utekelezaji Wa sheria ya kanuni za maadili zilifutwa rasmi mwaka 1992.
Viongozi waliweza kumiliki Mali kuwa na makampuni kuwa na majumba ya kupangisha, kuwa na mashamba makubwa wakasahau kauli ya "cheo ni dhamana" na kutotumia vyeo vyao na wengine kwa manufaa yao.
Matokeo yake kuuza Mali ya Umma mf viwanda, mashamba na Nyumba za serikali.
Leo hii Magufuli anatakaviwanda virejeshwe.
Tunakuwa washabiki na wasahaulifu kiasi cha kutohoji hapa tulipo sasa tumefikaje na tulikosea wapi!?

No comments: